3243; Vitu vinavyokupa ushindi.
Rafiki yangu mpendwa,
Msukumo wa kwanza kwetu kwenye chochote tunachofanya ni kupata ushindi.
Kila mtu anapenda ushindi, ni kiashiria kwamba mambo yamefanyika kwa usahihi.
Lakini watu ambao wamekuwa wanapata ushindi mzuri na unaodumu wamekuwa ni wachache sana.
Zipo sababu nyingi ambazo zimekuwa zinawakwamisha wengi wasipate ushindi mkubwa wanaoutaka.
Moja ya sababu kubwa inayowazuia wengi kupata ushindi ni kutokujua vitu sahihi vinavyoleta ushindi wanaotaka.
Wengi wanajikuta wakihangaika na mambo ambayo kwa nje yanaonekana ndiyo yanawapeleka kwenye ushindi, lakini kwa ndani mambo yanakuwa tofauti.
Wengi ambao hawapati ushindi wamekuwa wanahangaika na vitu ambavyo kwa nje vinaonekana kuwa vipya na vya tofauti.
Wanakuwa wanahangaika na vitu vinavyovutia na kusisimua kufanya.
Lakini ushindi halisi unatokana na kufanya mambo ya msingi kwa ukubwa na muda mrefu bila kuacha.
Mambo hayo ya msingi ndiyo yamekuwa yanapuuzwa na wengi ambao hukimbizana na mambo mapya na ya kusisimua kila mara.
Wanajikuta wakiwa wamefanya vitu vingi, lakini ushindi hakuna.
Tuangalie mfano kwenye eneo la biashara.
Unapata ushindi kwenye biashara kwa kufanya vitu vya msingi kwa ukubwa na msimamo.
Unakazana kuongeza mapato kwa kukuza mauzo ya biashara. Kwa kuwa mauzo ndiyo moyo wa biashara, yanapaswa kupewa kipaumbeke kikubwa.
Matumizi yanatakiwa kudhibitiwa ili yasimeze kipato chote. Huwa ni rahisi kwa matumizi kuongezeka pale mapato yanapoongezeka. Hilo linapotokea, ukuaji unakuwa mgumu.
Unatakiwa kuwa na timu nzuri ya watu wanaoiendesha biashara yako. Huwezi kufanya kila kitu peke yako kwenye biashara na ikapata mafanikio makubwa.
Unahitaji watu, na siyo tu watu ni watu, bali watu bora. Na hapa ndipo unapohitaji kuwa unaajiri vizuri.
Kuwajali sana wateja wa biashara ni kitu kingine cha msingi na muhimu kinachopaswa kufanyika.
Kila kinachofanywa kwenye biashara kinalenga kutoa thamani kubwa zaidi kwa wateja. Kwa umakini mkubwa kuwekwa kwa wateja, inakuwa rahisi kuwabakisha kwa muda mrefu na kuwavutia wengine.
Mwisho ni kujipa muda kwenye kila kinachoamuliwa kufanyika, kufanya kwa ukubwa na msimamo kwa muda mrefu bila kuacha.
Wengi wanashindwa siyo kwa sababu wanachofanya hakiwezekani, bali kwa sababu wanakuwa wamekata tamaa na kuacha kabla hawajafikia ushindi.
Rafiki, acha kuhangaika na vitu vya kusisimua ambavyo ndivyo kila mtu anahangaika navyo.
Badala yake fanya yale mambo ya msingi kwa ukubwa na msimamo.
Hayo ndiyo yatakayokupa ushindi mkubwa na wa ukahika mara zote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Wengi ambao wamekuwa hawapati ushindi wamekuwa wakihangaika na vitu ambavyo kwa nje vinaonekana kuwa vipya na vya tofauti.
LikeLike
Kabisa, wanapoteza sana muda.
LikeLike
Naacha kuhangaika na vitu vya kuleta msisimko badala yake naweka kazi kwenye vitu vitakavyonipatia ushindi wa kweli.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ushindi wa uhakika ni kufanya Yale ya msingi Kwa ukubwa na Kwa msimamo Kwa muda mrefu
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante sana kocha;
Ni kweli, wengi wanashindwa siyo kwa sababu wanachofanya hakiwezekani, bali kwa sababu wanakuwa wamekata tamaa na kuacha kabla hawajafikia ushindi. Nitakomaa mpaka mwisho, nipate ushindi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Matumizi yanatakiwa kudhibitiwa ili yasimeze kipato chote. Huwa ni rahisi kwa matumizi kuongezeka pale mapato yanapoongezeka. Hilo linapotokea, ukuaji unakuwa mgumu.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante sana kocha.
Ni kweli, kukata tamaa na kuishia njiani ni adui mkubwa wa Ushindi. Nitapambana, nitakuwa kinganganizi mpaka kieleweke.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Inahitaji watu,na sio watu tu,watu ni watu.
Bali watu bora.
Kuwajili Sana wateja wa biashara ni kitu kingine cha msingi na muhimu kinachopaswa kufanyika.
Kujipa muda kufanya ukubwa na msimamo kea muda mrefu bila kuacha.
🙏🙏
LikeLike
Tuzingatie hayo.
LikeLike
Asante Kocha,
Ili kujihakikishia ushindi mkubwa na wa uhakika mara zote nitafanya yale ya msingi kwa msimamo na kuachana na yale ya rahisi yenye kusisimua tu.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
_KUPATA USHINDI , ni msukumo wa kuweza kufanya chochote utakacho chagua kukufanya.
_ushindi halisi unatokana na kufanya Mambo ya msingi
kwa ukubwa na kwa muda mlefu
_sipaswi kuwa peke yangu ,ninahitaji watu Bora
_ili kupata matokeo bora ninapaswa kujipa muda ktk kile ninachofanya.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ushindi halisi unatokana na kufanya mambo ya msingi kwa ukubwa na muda mrefu bila kuacha,
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
ushindi halisi unatokana na kufanya mambo ya msingi kwa ukubwa na muda mrefu bila kuacha.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitafanya Mambo yanayonipa ushindi Mara zone.
LikeLike
Safi sana
LikeLike