3251; Unaowahofia siyo sahihi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kila tunapofanya jambo jipya na kubwa huwa unapatwa na hali ya hofu.
Hofu ni kiashiria kwamba unafanya kitu kikubwa au kipya kuliko ulivyozoea.
Wengi wamekuwa wanatumia hofu wanazokutana nazo kama sababu ya kuacha.
Lakini hilo halipaswi kuwa hivyo.
Hofu haipaswi kutufanya tuache.
Bali inapaswa kuwa kichocheo cha wewe kuendelea kufanya.
Hapa tunakwenda kuangalia ambazo siyo sahihi lakini zimekuwa kikwazo kwa wengi.
Na kubwa katika aina hizo za hofu ni hofu ya wengine watakuchukujiaje.
Pale unapopanga kuchukua hatua fulani, lakini inapofika kwenye kufanya unahofia wengine watakuchukuliaje, hupaswi kusikiliza na kuacha.
Kila unapopatwa na hofu ya wengine watakuchukuliaje, unapaswa kuhakikisha unaendelea kuchukua hatua kama ulivyopanga.
Hiyo ni kwa sababu hofu ya wengine watakuchukuliaje ndiyo hofu uongo na dhaifu kuliko zote.
Lakini pia ndiyo hofu ambayo imekuwa inawakwamisha wengi kupiga hatua.
Hofu ya wengine watakuchukuliaje siyo sahihi kwa sababu;
1. Watu wengi hawakufikirii kama unavyodhani, kila mtu ana yake anayohangaika nayo kwenye maisha.
2. Wale wanaokufikiria, wanakufikiria mema zaidi kuliko mabaya.
3. Kama mtu anapata muda wa kutosha kufuatilia kila kitu kwenye maisha yako, huenda pia siyo mtu sahihi wa kumsikiliza, kwa sababu hana makubwa anayohangaika nayo.
Watu wengi ambao hawajafanikiwa, huwa wanakwama kufanikiwa kwa sababu wanahofia wengine ambao nao hawajafanikiwa watawachukuliaje.
Yaani unakwama kufanikiwa kwa sababu hutaki kuwaudhi ambao hawajafanikiwa.
Hilo siyo sahihi hata kidogo.
Usikubali kukwama kwenye jambo lolote, kwa sababu ya watu ambao nao hawajafanikiwa kwenye jambo hilo.
Hofu yoyote inayowahusu watu siyo hofu sahihi, usiisikilize wala kuifuata, bali ipuuze na endelea kufanya.
Endelea kufanya licha ya hofu unazokuwa unakutana nazo na utaweza kufanya makubwa.
Muhimu sana ni pale unapohofia wengine watakuchukukuliaje, kwanza jiulize ni makubwa gani wamefanya kwenye maisha yako.
Ambao wameshaweza kufanya makubwa, huwa hawana hata muda wa kufuatilia wengine. Na kama itatoka wakafuatilia wengine, huwa na mategemeo mazuri kwao.
Wakwamishaji wakubwa ni wale ambao hakuna makubwa waliyoweza kufanya kwenye maisha yao.
Hao ndiyo wanakuwa wakatishaji tamaa wakubwa.
Kwa kuwa wao wameshindwa, wanaamini wengine nao watashindwa.
Hawa wapuuze kabisa, usichukue chochote kwao.
Dawa ya hofu ni kufanya.
Na dawa ya hofu ya wengine watakuchukuliaje ni kuipuuza kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Sipaswi kumfhofia mtu yeyote kwa sababu, unayemfia pia ana hofu zake. au muda mwingine anakuhofia wewe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Dawa ya hofu ni kufanya …. Nakupuuza wengine wanakuchuliaje
Asante sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Dawa ya hofu ni kufanya.
Na dawa ya hofu ya wengine watakuchukuliaje ni kuipuuza kabisa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wakwamishaji wakubwa ni wale ambao hakuna makubwa waliyoweza kufanya kwenye maisha yao.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Dawa ya hofu ni kufanya.
Dawa ya hofu wengine wanakuchukuliaje ni kuipuuza.
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Dawa ya hofu ni kufanya na kupuuzwa yanayosemwa na wengine
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Wanaowafikiria vibaya wengine wengi wao hawajafanya makubwa yoyote.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Dawa ya wote ni kuipuuz
Namini w8
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Una Hofu ya kufanikiwa kwa sababu ya kuwaogopa ambao hawajafanikiwa
LikeLike
Jambo la kushangaza.
LikeLike
Umuhimu mkubwa wa kupuuza ili kupiga hatua zaidi kwenye maisha na kuwa imara
LikeLike
Kabisa.
LikeLike