3255; Uhakika wa ushindi.

Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu ambao wana uhakika wa ushindi kwenye maisha yao.
Siyo kwa sababu mambo yanakuwa rahisi ila kwa sababu wao wanakuwa wagumu kiasi kwamba hakuna kinachoweza kuwazuia kufanikiwa.

Maisha yanaweza kuwachelewesha.
Maisha yanaweza kuwachanganya.
Lakini ile nia yao ya ushindi haifi kamwe.
Ni nia hiyo ndiyo inayoendelea kuwasukuma mpaka kupata ushindi mkubwa.

Nia kubwa ya ushindi wanayokuwa nayo ndiyo inawapa msukumo wa kuchukua hatua kubwa bila kuchoka.

Kuchukua hatua kubwa bila ya kuchoka kunawakutanisha na fursa mbalimbali ambazo zinachangia kwenye mafanikio wanayoyataka.

Watu hao wanapopata mafanikio makubwa, kwa nje inaonekana kama ni rahisi.
Inaweza kuonekana pia ni kama bahati.

Lakini ambacho wengi hawaoni ni yale yanayokuwa yanaendelea nyuma ya pazia kwa kipindi kirefu kabla ya mafanikio hayo.

Haijalishi mtu anakuwa anapotia magumu na changamoto nyingi kiasi gani, swala la kupata ushindi halifutiki kwenye fikra zao.
Wanajua kwa hakika kwamba watapata ushindi na hilo kwao linakuwa swala la muda tu.

Je wewe ni uhakika kiasi gani umejiwekea kwenye kupata ushindi unaoutaka?
Umejitoa kiasi gani kwenye kufanya kwa mwendelezo bila ya kuacha?
Unakabilianaje na magumu na changamoto unazokutana nazo?
Majibu sahihi ya maswali hayo ndiyo yanakupa picha ya uhakika wa mafanikio kwako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe