3266; Kwa nini huna imani?
Rafiki yangu mpendwa,
Hivi karibuni kuna mtu aliniandikia akiomba ushauri ni biashara gani ya mtaji mdogo anayoweza kuifanya na ikampa faida kubwa?
Kama kawaida yangu, huwa sikimbilii kumwambia mtu nini afanye, bali namuuliza kwanza maswali ili kumwelewa kwa kina.
Na kupitia kumuuliza maswali mtu huyo niligundua tayari kuna biashara anafanya.
Na hapo ndipo nilipomuuliza swali moja muhimu sana, ambalo pia nataka kukuuliza wewe hapa. Nilimuuliza; “Kwa nini unatafuta biashara nyingine ya kufanya yenye faida kubwa badala ya kukuza hiyo uliyonayo sasa?”
Hili ni swali ambalo nakuuliza na wewe rafiki yangu, ambaye kuna biashara tayari unaifanya sasa, lakini unatafuta biashara nyingine ya kufanya.
Au unafanya biashara zaidi ya moja kwa sasa na zote zinakutegemea wewe moja kwa moja.
Ila kwako nitalirahisisha zaidi hilo swali, ili likusaidie kufanya maamuzi.
Swali ninalokuuliza wewe rafiki yangu ni; “Kwa nini huna imani?”
Kwa nini huna imani kwamba biashara unayofanya sasa inaweza kukupa mafanikio makubwa mpaka unatafuta nyingine ya kufanya?
Kwa nini huna imani ya kuweka juhudi zako zote kwenye biashara moja mpaka ifanikiwe kabla ya kutawanya kwenye biashara nyingi ambazo zinakutegemea?
Rafiki, kadiri unavyohangaika na mambo mengi, unaonyesha jinsi ulivyokosa imani kwenye jambo lolote moja.
Najua unachofikiria ni unahitaji kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Na utaonyesha kwa mifano jinsi ambavyo wale wenye utajiri mkubwa wana vyanzo vingi vya kipato.
Kitu ambacho utakuwa hujui, au kama unajua basi unajisahaulisha ni kwamba hao wenye utajiri mkubwa unaowaona sasa wana vyanzo vingi vya kipato hawakuanza vyote kwa pamoja.
Badala yake walianza na chanzo kimoja, wakakifanyia kazi kwa umakini mkubwa mpaka kikawa cha uhakika na kisichowategemea. Ndipo wakaenda kwenye vyanzo vingine.
Turudi kwako rafiki yangu, kwenye swali kuu la ukurasa huu wa leo; Kwa nini huna imani kwenye hicho unachofanya sasa mpaka unatamani kufanya vitu vingine au unafanya vingi kwa pamoja?
Karibu ushirikishe majibu yako hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
“kadiri unavyohangaika na mambo mengi, unaonyesha jinsi ulivyokosa imani kwenye jambo lolote moja.”
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nafikiri ni ujinga ulikuwa unanisumbua, sasa nimebadilika.
LikeLike
Safi sana,
Usirudi tena kwenye huo ujinga.
LikeLike
Asante Kocha,
Nilikuwa sitendi kwa msimamo, nilifuata mkumbo, nilidhani hadhi (kama msomi hufai kufanya shughuli fulani i.e kuona aibu/haya) ni muhimu kwenye kutafuta riziki. Kwa ujumla niliongozwa na msukumo wa nnje.
Kwenye KCM nimejifunza masoko, mfumo, mauzo (ushawishi). Zaidi ni kujenga tabia ya kujifunza, hasa kwa kusoma. Nimekuwa sasa wa kujiuliza KWA NINI, tena KWA NINI KUBWA. Nikifanya maaumuzi ninaweka mipango, lengo; kisha ninakaa kwenye mchakato kwa msimamo na furaha. Ninaufanyia kazi mrejesho na kyapokea matokeo jinsi yalivyo bila kuwa na msongo. Fikra ni kuendelea kuboresha daima.
LikeLike
Vizuri sana,
Kaa humu bila kuyumba.
LikeLike
Mimi ni kwasababu ya kukosa uvumilivu, nilitaka kupata faida ya haraka haraka, hivyo niliona hii inachelewa. Kwa kufanya biashara nyingi nyingi niliona hata hii ikichelewa au ikifa nitakuwa na pa kuanzia. Hii yote ni kukosa Imani.
Ili nimejifunza kuanzia Leo nitakuwa mvumilivu kujenga biashara Moja Hadi ikue na iweze kujiendesha yenyewe bila kunitegemea kabisa.
LikeLike
Vizuri, uvumilivu unalipa sana.
Tuwe na Imani.
LikeLike
Ni kweli kwa kutokua na imani ndiyo maana unatangatanga na sasa ukiangalia na wengine unavhanganyikiwa zaidi mimi nimeamua kuweka imani kwenye biashara hii moja na kuweka pembeni vingine vyote na sasa naamua kuopelekahadi inipe utajiri mkubwa na kuweza kujiendeshayenyewe nimeweka lengo kubwa la kuniwezesha kupata uhuru huo kabla ya kuingia kwenye biaahara nyingine yoyote na Mungu anisaidie niweze kuuona huku napambana
LikeLike
Vizuri sana kwa maamuzi hayo.
Kila la kheri.
LikeLike
Ili uweze kumiliki vyanzo vingi vya kipato lazima usimamie chanzo kimoja mpaka kiweze kujitegemea ndipo uende chanzo kinginge
Asante sana
LikeLike
Kabisa, nguvu zote ziende kwenye kitu kimoja kwa uhakika kabla ya kutawanya.
LikeLike
Nikae kwenye biashara moja na kwa muda mrefu mpaka ifanikiwe!
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Utulivu na uvumilivu kwenye biashara ni muhimu sana ktk ukuaji wa biashara.
LikeLike
Kabisa, bila utulivu safari inakuwa ngumu sana.
LikeLike