3279; Uhakika wa ushindi.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wamekuwa wanahangaika sana kupata ushindi, lakini wamekuwa hawaupati.
Hiyo ni kwa sababu wengi wamekuwa hawauelewi ushindi.
Wanahangaika na mengi na kutaka kupata matokeo makubwa na ya haraka.
Wakichelewa kupata matokeo wanayotaka, wanaacha na kwenda kwenye kitu kingine.
Uhakika wa ushindi siyo kupata kile unachotaka, bali kutokuacha kufanya kile unachofanya ili kupata ushindi.
Kama utafanya kitu kwa muda mrefu zaidi, kupata ushindi ni uhakika kabisa.
Wengi wanakosa ushindi kwa sababu wanaacha kufanya mapema.
Kama wangeendelea wangeweza kukutana na fursa nzuri ya kushinda.
Lakini wanakuwa wameacha mapema.
Lakini pia wengi wanadhani ushindi ni kufanya mambo makubwa na magumu.
Wanahangaika na hayo na bado hawashindi.
Ukweli ni ushindi ni kufanya mambo rahisi na ya msingi, kwa msimamo bila kuacha.
Kwa kufanya yale mambo ya msingi kabisa mara zote, matokeo makubwa na ya tofauti yanapatikana.
Kwa vigezo hivi viwili vya ushindi tulivyoona, vinafanya ushindani kuwa mdogo sana.
Siyo kwa sababu ushindi ni mgumu, bali kwa sababu wengi ni wepesi sana na hawawezi kukabiliana na hali hizo.
Watu wengi hawawezi kufanya kitu kwa muda mrefu, hasa kama hawaoni matokeo ya haraka.
Hivyo wengi wanaacha haraka kufanya na kuacha uwanja wa ushindani ukiwa tupu.
Kama utajiambia tu kwamba huachi kufanya hata iweje, huo tayari ni ushindi.
Maana wengi hawawezi hilo.
Na pia, wengi hudhani kama kitu siyo kigumu basi hakiwezi kuleta matokeo makubwa.
Hivyo huwa wanahangaika na magumu ambayo yanawachosha na kuwapoteza.
Wewe ukisimamia yale ya msingi, ambayo pia ni rahisi, unakuwa mbele sana ya hao wengine.
Ushindi ni wa uhakika kwako kama utayazingatia hayo ya msingi kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kutokuacha kufanya yale ya msingi kabisa hata iweje kwa muda mrefu hadi ushindi upatikame hayo ya msingi ni mchakato kwa msimamo bola kuacha pia uwekezaji kwa msimamp bila kuacha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ushindi ni kufanya mambo rahisi na ya msingi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kuendelea kufanya jambo lolote lenye tija kwa msimamo ni kigezo moja wapo cha kuelekea kwenye ushindi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ya msingi na rahisi.Nitafanya kwa msimamo siku zote.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ushindi ni kufanya na kufanya Mambo rahisi na ya msingi kwa msimamo bila kuacha.utajikuta uwanja mtupu na ushindani bye bye.
🙏🙏🙏
LikeLike
Kabisa, watachoka wote na kukuacha.
LikeLike
Kama utajiambia tu kwamba huachi kufanya hata iweje, huo tayari ni ushindi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ili kupata ushindi wa uhakika kufanya kila siku
Asante
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante kocha, Kumbe kuendelea kubaki hapa ni ushindi
Tayar kwa kuendelea kwa msimamo thabiti
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
ahahahahaha kumbe,,,
Uhakika wa ushindi sio kupata ushindi bali ni kutokuacha kufanya kile unachofanya ili kupata ushindi,
Nimekusoma kocha Makirita
LikeLike
Vizuri sana, kuwa wa mwisho kubaki umesimama baada ya wengine wote kuchemka.
LikeLike