3280; Kwa msimamo bila kuacha.

Rafiki yangu mpendwa,
Inapokuja kwenye mafanikio, watu wanaijua kanuni ya mtu kujua kile hasa unachotaka na unachopaswa kufanya ili kukipata.

Na watu wanafanya hivyo kweli.
Wanakuwa wanaju mafanikio wanayotaka kuyapata.
Na pia wanajua wanachopaswa kufanya ili kuyapata.
Na hata kufanya wanafanya.
Lakini hawayapati mafanikio waliyotegemea kuyapata.

Kinachokuwa kimewakwamisha ni kutozingatia hitaji muhimu kwenye ufanyaji.
Ambalo ni kufanya kwa msimamo bila kuacha, hata kama matokeo hayaji vile mtu umetarajia.

Ingekuwa kuanza kufanya ndiyo mafanikio, wengi sana wangekuwa na mafanikio.
Maana wengi ni waanzaji wa kufanya.
Lakini wanapokutana na ugumu,
Au matokeo waliyotegemea yanapochelewa,
Wanaacha kufanya.

Kitu kingine muhimu kwenye kufanya kwa msimamo bila kuacha ni kufanya yale ya msingi.
Maana pengine ambapo wengi wanakwama ni kukimbizana na mambo mapya kila wakati.
Watu wanaposikia kitu chochote kipya, wanaona hicho ndiyo cha uhakika zaidi.
Wanakimbilia kukifanya na kuacha walichokuwa wanafanya.
Haiwachukui muda kwenye hicho, wanaona kingine kipya na kukiendea pia.

Hivyo kufanya kwa msimamo bila kuacha inahusisha kufanya kile ambacho umeshachagua kufanya na kupuuza mengi mapya yanayojitokeza.

Watu pia wanapenda kuhangaika na mambo makubwa na magumu.
Wakiamini hayo ndiyo yenye mafanikio ya uhakika.
Lakini bado hawapati kile wanachokuwa wanakitaka.

Kufanya kwa msimamo bila kuacha, hata kwa vitu ambavyo ni rahisi kabisa kuna nguvu kubwa ya kuleta matokeo makubwa na ya uhakika.

Mafanikio makubwa yanakutaka sana mtu ufanye yale ya msingi kwa msimamo bila kuacha na bila ya huruma yoyote.

Unapofanya kwa msimamo bila kuacha, unajijengea sifa ya kuaminiwa na kutegemewa na wengi kwenye kile unachofanya.
Ni imani na utegemezi huo ndiyo vinakuhakikishia mafanikio makubwa.

Nini ambacho wewe umechagua kufanya kwa msimamo bila kuacha?
Shirikisha kwenye maoni hapo chini.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe