3298; Hatari kubwa zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Hatari kubwa zaidi kwa mtu ni kupata kile anachotaka kwa haraka na urahisi bila ya kuingia gharama yoyote ile.
Hiyo huwa ni hatari kubwa na inayoharibu kabisa maisha ya mtu kwa sababu inamfanya ajione ana uwezo mkubwa kuliko uhalisia wake.
Kwa kuwa mtu anakuwa amepata kitu kwa ukubwa na haraka bila ya kuingia gharama yoyote, anavipoteza vitu hivyo kwa urahisi na haraka bila ya kuingia manufaa yoyote.
Mtu anakuwa amepata kitu kabla ya kuwa na maandalizi sahihi ya kukabili kitu hicho.
Na kwa sababu matokeo makubwa huwa yanakuja na wajibu mkubwa, mtu anakuwa hajajiandaa kuwajibika.
Mifano ipo mingi ya watu waliopata fedha nyingi kwa haraka na bila ya kuingia gharama ya kuweka kazi.
Wanaoshinda bahati nasibu, wanaopata urithi, mafao na mengine.
Mwisho wao umekuwa siyo mzuri mara zote.
Lakini pia hata wanaopata nafasi kubwa kama za uongozi bila ya kuingia gharama ya kuweka kazi.
Wamekuwa wanazitumia vibaya na kuleta uharibifu mkubwa.
Wakati unapambana kupata kile unachotaka, unaweza kutamani sana upate kwa urahisi na haraka.
Lakini omba sana hilo lisitokee, maana litaharibu kabisa maisha yako.
Lipa gharama sahihi ya kile unachotaka, gharama ya kazi na muda. Na pale unapolipa gharama ya kutosha, unapopata kitu kinakuwa na manufaa kwako.
Furahia kulipa gharama ya kila unachotaka, inakujengea nidhamu kubwa sana kwenye kukitumia na kunufaika nacho.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Matokeo makubwa yanakuja na wajibu mkubwa
Asante sana
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Furahia kulipa gharama ya kila unachotaka, inakujengea nidhamu kubwa sana kwenye kukitumia na kunufaika nacho.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Lipa gharama sahihi ya kile unachotaka, nitaendelea kupambana kwa kulipa gharama
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Chochote kinachopatikana bila kuweka kazi Wala muda hakina thamani na kina hatari kubwa ya kupotea
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Lipa gharama halisi ya kuwekeza kwenye unachokitaka. Fuata mchakato sahihi ili ufikie mafanikio yake
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Lipa gharama sahihi ya kile unachotaka yaani gharama ya kazi na muda ili unapokipata kiwe na thamani kwako.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kulipa gharama sahihi ya kile unachotaka kwa maana ya kazi na muda.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike