Watu wengi wanaoutaka utajiri ila hawaupati, siyo kwa sababu hawawezi kuupata, bali ni kwa sababu hawajui njia sahihi za kuupata. Na kwa sababu hakuna kokote ambapo somo la utajiri linafundishwa, si nyumbani wala shuleni, watu wanaenda maisha yao yote wakibahatisha kwenye kujenga utajiri.

Hilo ndiyo limesababisha watu kujikuta wakifanya mambo ambayo siyo tu yanawanyima utajiri, bali pia yanakuwa kikwazo kwao kujenga utajiri kwenye siku zijazo. Kwa mfano watu wanajikuta wakiingia kwenye madeni makubwa ambao wanayalipa kwa muda mrefu na kuwa kikwazo kwao kujenga utajiri.

Kanuni ya uhakika ya kujenga utajiri na inayofanya kazi kwa watu wote ni hii; ONGEZA KIPATO, DHIBITI MATUMIZI, WEKA AKIBA NA IWEKEZE AKIBA HIYO KWA MUDA MREFU BILA KUINGILIA UWEKEZAJI WAKO.

Sentensi hiyo moja inaweza kutoa maelfu ya vitabu, inaweza kukuingia gharama kubwa kwenda kujifunza, lakini utarudi hapo hapo.

Kujenga utajiri lazima uanze na kipato. Na siyo tu kipato, bali kipato kinachoenda kikiongezeka kadiri muda unavyokwenda.

Kila mtu mzima anayeishi maisha ya kujitegemea tayari ana njia ya kuingiza kipato. Lakini kwa nini wengi siyo matajiri? Sababu ni kikwazo kikuu cha utajiri ambacho ni matumizi. Fedha ikiwepo huwa haikosi matumizi. Na hapo ndipo swala la kudhibiti matumizi linapohitajika kwenye safari ya kujenga utajiri.

Hivyo kwa kila kipato ambacho mtu anaingiza, anatakiwa kuweka akiba kwanza kabla ya kufanya matumizi. Badala ya kufanya matumizi halafu kinachobaki kuweka akiba, mtu unapaswa kuweka akiba kwanza kisha kinachobaki unafanya matumizi.

Kuweka akiba tu hakutoshi kujenga utajiri, bali akiba hiyo inatakiwa nayo iweze kuzalisha. Na hapo ndipo uwekezaji unapohitajika kufanyika ili kutumia akiba kujenga utajiri.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeelezea kwa kina upande wa kipato, ambayo ndiyo mbegu kuu ya kujenga utajiri. Nimeeleza aina za kipato na kwenye kila aina jinsi ya kuongeza kipato hicho kwa ukubwa zaidi.

Karibu uangalie kipindi hiki, ujifunze na uende ukachukue hatua ili ukuze kipato chako na kuweza kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yako.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.