Huwa hatuoni vitu kwa jinsi vilivyo, bali tunaona vitu kwa jinsi sisi tulivyo. Watu wawili, walio kwenye eneo moja na wakashuhudia tukio moja, bado kila mmoja atakuwa na tafsiri yake ya tofauti kuhusu tukio hilo. Hiyo ni kwa sababu wanavyotafsiri kitu inatokana na wao wenyewe na siyo jinsi kitu kilivyo.

Kwenye mauzo, mtazamo ambao muuzaji anakuwa nao huwa una athari kubwa kwenye matokeo anayopata. Nyakati huwa hazilingani, kuna vipindi mauzo huwa yanakuwa juu na wakati mwingine kuwa chini. Wauzaji ambao ni bora huwa wanafanya mauzo makubwa kwenye vipindi vyote. Hiyo ni kwa sababu namna wanavyoyachukulia mauzo ni tofauti kabisa na wauzaji wengine.

Ili uweze kuwa muuzaji bora na kufanya mauzo makubwa wakati wote, kuna aina ya mtazamo wa tofauti unaopaswa kujijengea. Mtazamo huo ni tofauti kabisa na ulionao sasa, ambao umekukwamisha kwa muda mrefu.

Kwenye kipindi cha video hapo chini nimekushirikisha kwa kina mtazamo huo unaopaswa kuujenga na hatua za kuchukua ili kuhakikisha umejenga mtazamo huo na kunufaika nao. Karibu ujifunze na kunufaika.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.