Rafiki yangu mpendwa,

Watu wengi huwa wanasema wanauchukia umasikini, lakini hawaonekani kumaanisha kweli hilo. Hiyo ni kwa sababu licha ya watu hao kusema hawautaki umasikini, bado wanakuwa wameukumbatia utumwa wa kifedha, ambao unawafanya wabaki kwenye umasikini.

Matoke kwenye maisha huwa hayaji kwa maneno ambayo mtu anasema, bali yanachangiwa na matendo ambayo mtu anafanya. Hivyo mtu kusema anauchukia umasikini, wakati matendo yake ni tofauti, haiwezi kumwondoa kwenye umasikini huo.

Kadhalika kwenye kutaka kuongeza kipato na kujenga utajiri, wengi wanasema wanataka hivyo. Lakini matendo yao hayawezi kuwapa hicho wanachotaka.

Kama kweli unataka kutoka kwenye umasikini na kuelekea kwenye utajiri, hatua ya kwanza unayopaswa kuchukua ni kuacha kukumbatia utumwa wa kifedha ambao unao sasa.

Utumwa huo wa kifedha ni kipato chako kuwa cha moja kwa moja, yaani inabidi ufanye kazi au biashara ndiyo uingize kipato. Unaweza kushangaa kuhusu hili, kwamba si ndiyo watu wanavyopaswa kuingiza kipato?

Ni kweli, watu wanaingiza kipato kwa kufanya kazi au biashara, lakini hao ndiyo wanaobaki kwenye umasikini au kushindwa kujenga utajiri mkubwa. Wale wanaoondoka kwenye umasikini na kuweza kujenga utajiri mkubwa ni wanaojenga mfumo unaowaingizia kipato bila wao kulazimika kufanya kazi au biashara moja kwa moja.

Bilionea Warren Buffett amewahi kunukuliwa akisema kama huwezi kuifanya fedha ikufanyie kazi, utafanya kazi maisha yako yote. Kwa bahati mbaya sana hivyo ndivyo wengi wanavyoyaendesha maisha yao na ndiyo maana yanakuwa magumu.

kama kweli umedhamiria kuondoka kwenye umasikini basi unapaswa kuanza mara moja kuondoka kwenye huo utumwa wa kipato chako kutegemea ufanyaji wako wa moja kwa moja.

Swali zuri unalojiuliza ni unawezaje kufanya hivyo? Vizuri, majibu ya swali hilo yapo kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo nimefafanua kwa kina dhana hii ya utumwa wa kifedha na njia ya uhakika ya kutoka kwenye utumwa huo. Karibu uangalie kipindi hiki, ujifunze na kuchukua hatua ili uweze kuondoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri ambao unautaka kwenye maisha yako.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.