Rafiki yangu mpendwa,
Takwimu za biashara huwa zimekuwa ni za kuumiza na kusikitisha. Takwimu hizo zimekuwa zinaonyesha zaidi ya nusu ya biashara mpya zinazoanzishwa, huwa zinakufa ndani ya mwaka mmoja.
Ukisikia takwimu za aina hiyo, unaweza usielewe sana kama haupo kwenye biashara. Lakini unapokuwa kwenye biashara, kwa kujua ugumu na changamoto zake, inakuumiza sana.
Ni sawa na mtu anayejua uchungu wa uzazi, halafu aambiwe mtoto aliyemzaa ana uwezekano mkubwa wa kufa ndani ya mwaka mmoja.

Huo ndiyo uhalisia uliopo kwenye biashara, nyingi mpya zinazoanzishwa zinakufa ndani ya muda mfupi.
Na hata kwa zile ambazo hazifi, bado zimekuwa hazipati ukuaji mkubwa kama ambavyo waanzilishi wa biashara hizo walitegemea. Zinabaki kwenye hali ya kudumaa na kushindwa kuleta matokeo makubwa.
Zipo sababu nyingi zinazopelekea biashara nyingi kufa, lakini kuna saba ambazo zimekuwa zinajirudia rudia kwenye biashara nyingi zinazokufa.
Sababu hizo saba zimeelezewa kwa kina kwenye kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA, ambacho unakipata kwa KUBONYEZA MAANDISHI HAYA.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimezifafanua sababu hizo saba zinazoua biashara nyingi na jinsi unavyoweza kuziepuka ili biashara uliyonayo au unayopanga kuanzisha isife kama nyingi zinavyokufa.
Sehemu kubwa ya sababu zinazoua biashara nyingi zimekuwa zinaanzia ndani ya biashara yenyewe kuliko nje. Pale biashara inapokufa, wengi huangalia sababu za nje kama ushindani, hali ya uchumi na nyinginezo. Lakini ukweli ni kifo huwa kinaanzia ndani, nje huwa kunamalizia tu.
Fungua kipindi hapo chini na ujifunze ili uweze kujenga biashara itakayodumu kwa muda mrefu na kukupa mafanikio makubwa kama unavyotaka.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.