Rafiki yangu mpendwa,

Leo nataka nikurudishe maisha ya shuleni kidogo, nikukumbushe mambo uliyosumbuliwa nayo sana, ukaadhibiwa kwa kutoyajua, ukafeli mitihani kwa sababu hukuyajua, lakini leo hii huyatumii kabisa.

1. Mto mrefu kuliko yote duniani ni upi?

2. Mlima mrefu zaidi duniani ni upi?

3. Vita ya majimaji ilipiganwa mwaka gani?

4. Nani wa kwanza kugundua mlima Kilimanjaro?

5. Taja aina za miamba.

Rafiki, hayo ulihangaishwa nayo sana wakati uko shuleni, lakini leo hii ni mangapi ambayo unayatumia kwenye maisha yako ya kila siku? Kujua mtu wa kwanza kugundua mlima Kilimanjaro, imekusaidiaje kwenye kuendesha maisha yako ya jana?

Sisemi hayo tuliyojifunza hayana umuhimu kabisa, umuhimu upo wa kujua historia yetu, jografia, sayansi na mengine ya msingi.

Tatizo ni kwamba kuna mambo ya msingi sana, ambayo unahangaika nayo kila siku, lakini shuleni hukufundishwa kabisa.

Kuna kitu ambacho unakifikiria muda wote, ukienda kulala unakiota, ukiamka unaanza nacho, lakini hukufundishwa kabisa.

Kitu ambacho kinakusumbua kwa maisha yako yote, hukuwahi kukaa darasani na kufundishwa misingi yake.

Na matokeo yake ni kuwa na maisha ya mateso yanayosababishwa na makosa unayoyafanya kwenye eneo hilo kwa kukosa elimu ya msingi.

Rafiki, ninachoongelea hapa ni FEDHA, ambayo ndiyo tuna matumizi nayo ya kila siku, lakini hatukuwahi kupewa elimu ya msingi juu yake.

Sehemu kubwa ya yale unayoyafanya kwenye fedha ni kwa kuiga au mazoea binafsi. Kwa sehemu kubwa, hujawahi kukaa chini na kufundishwa misingi ya fedha binafsi, ambayo ni muhimu mno.

Rafiki, hebu fikiria mambo ya msingi kama haya ambayo huenda huyajui na yanakuumiza;

1. Kuweka bajeti ya matumizi ya fedha binafsi.

2. Tofauti ya madeni mazuri na madeni mabaya.

3. Uwekezaji kwenye soko la hisa.

4. Uwekezaji kwenye hatifungani.

5. Kufanya fedha ikufanyie wewe kazi.

Ni mangapi kati ya hayo unaweza kuyaelezea kwa kujiamini mbele ya watu wengine?

Ni mangapi kati ya hayo unayafanyia kazi kwa vitendo?

Rafiki, kama unaanza ukiwa huyajui hayo au huyafanyi kwa vitendo, linaweza lisiwe tatizo lako, kwa sababu hukufundishwa shuleni.

Lakini kama utaendelea na maisha yako bila ya kuyajua hayo, linakuwa ni kosa lako kabisa, kwa sababu zipo fursa za wewe kujifunza na kuchukua hatua za tofauti.

SOMA; Je Ukipata Fedha Mawazo Mazuri Yanapotea?…

Na kama hujui wapi pa kuanza kujifunza, kipo kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, ambacho kimekupa elimu hiyo kwa lugha rahisi kwako kuelewa na hatua za kuanza kuchukua mara moja ili kunufaika.

Kitabu cha ELIMU YA FEDHA ni cha msingi ambacho kila mtu aliye makini na fedha zake anapaswa kuwa nazo. Kama mpaka sasa huna kitabu hicho, hebu chukua hatua mara moja sasa. Wasiliana na namba 0678977007 kupata nakala yako ya kitabu.

Rafiki, umeshakuwa mtu mzima, kulaumu mifumo ambayo haikukupa elimu hii muhimu hakutakusaidia. Badala yake unapaswa kushika hatamu ya maisha yako, kwa kujifunza na kuchukua hatua ili uwe vizuri kwenye eneo hilo muhimu la fedha.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimekuonyesha yale unayokwenda kuyapata kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Fungua uangalie na kujifunza. Kupata kitabu wasiliana na namba 0678977007.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.