3398; Furahia ugumu.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Wakati watu wengi wanakimbia na kulalamikia ugumu wa safari ya mafanikio, wewe unapaswa kuwa unaufurahia ugumu huo.
Hiyo ni kwa sababu kitu chochote chenye thamani kufanya, huwa ni kigumu kufanya.
Kadiri thamani ya kitu inavyokuwa kubwa, ndivyo ufanyaji unakuwa mgumu pia.
Kadiri matokeo yanavyokuwa makubwa, ndivyo ufanyaji unakuwa mgumu.
Kufurahia ugumu ndiyo njia ya kukutofautisha na walio wengi.
Kwa sababu wengi huwa hawapendi ugumu.
Kwa sababu wengi hukimbilia urahisi, wachache sana ndiyo wanaonaki kwenye ugumu.
Hilo linafanya ushindani kuwa mdogo kwenye ugumu.
Ushindani kuwa mdogo kunakupa fursa ya kupata matokeo makubwa na mazuri zaidi.
Lakini pia ugumu ni muhimu ili mtu kupata hali ya kuridhika.
Vitu vinapokuwa rahisi huwa hatuvithamini sana.
Na hivyo tunaishia kuvipoteza na kutokunufaika navyo.
Wakati wa kufanya tumekuwa tunatafuta vile rahisi kufanya.
Lakini kwenye kukumbuka vitu ambavyo vimekuwa na maana na mchango kwenye maisha yetu, tunaangalia vile ambavyo vilikuwa vigumu zaidi.
Vitu rahisi kufanya huwa vinatupa raha ya muda mfupi.
Lakini kadiri muda unavyokwenda, ndivyo tunavyochoshwa na pia kujisikia vibaya kwa mambo rahisi tunayokuwa tumehangaika nayo.
Hata kwenye kujisifia na kujivunia na vitu ambavyo mtu umefanya, utatumia vile vigumu zaidi kuliko ambavyo ni rahisi.
Unajua kabisa hakuna mtu atakayekupa umakini mkubwa kama umepata matokeo yako kwa njia ambazo ni rahisi.
Chochote kinachokutofautisha na kundi kubwa la watu ni cha kufurahia na kuthamini.
Kwa sababu wengi huwa hawapo sahihi, kwenye kupata mafanikio makubwa.
Unapokuwa tayari kuweka kazi na subira, utaweza kuvuka kila aina ya ugumu na kupata matokeo ambayo kwa wengine ni ndoto tu.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe