Rafiki yangu mpendwa,

Moja ya changamoto ambayo wanaoanzisha biashara wakiwa kwenye ajira wanakutana nayo ni kuibiwa. Kwa kuwa muda mwingi mtu anakuwa hayupo kwenye biashara, analazimika kuwaachia watu wengine waiendeshe. Hapo ndipo matatizo huanzia.

Kwa kuona changamoto ni kubwa kwa watu baki, watu huona ni bora wawape watu wao wa karibu wasimamie biashara zao. Lakini hilo nalo limekuwa halisaidii, kwani hata watu wa karibu nao huwa wanaishia kuwaibia kwenye biashara.

Jambo la kusikitisha ni mpaka hata watu wa ndani ya familia, wamekuwa wanaziumiza saba biashara, wakati mwingine bila hata ya kujua.

Hivyo kwa kutegemea watu wajitambue wenyewe na kuwa na uchungu na biashara yako, huwezi kufanikiwa kwenye biashara wakati unaendelea na ajira yako.

Kwa bahati nzuri sana, lipo suluhisho la kuzuia usiibiwe kwenye biashara unayoanzisha ukiwa kwenye ajira.

Kwenye kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, unapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kujenga mfumo wa kuiendesha biashara yako ambao unaondoa mianya yote ya wizi kwenye biashara.

Kwa mfumo ambao unauweka, kila mtu kwenye biashara anakuwa na majukumu yake ambayo anapimwa kwa namba. Hilo litakusaidia wewe kuweka uwajibikaji kwenye biashara na kuweza kupima uzalishaji na ufanisi wa kila mtu.

Lakini pia mfumo unakuwa na njia ya kudhibiti mzunguko wa fedha kwenye biashara. Tatizo la fedha ni huwa zinaibua tamaa. Mtu anapoona fedha ipo tu na akiichukua hawezi kujulikana, ataichukua na kuhalalisha kwa shida alizonazo. Njia ya kuondokana na hilo ni kuwa na udhibiti wa mzunguko wa fedha ambapo kunakuwa hakuna mwanya wa mtu kuchukua hata shilingi mia moja na isijulikane.

SOMA; BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira.

Kitu kikubwa zaidi ambacho kitahitajika kwenye biashara ni macho ya ziada, hapa namaanisha kamera ambazo zinakuwa eneo la biashara na wewe kuweza kuangalia kinachoendelea ukiwa popote pale. Watu wanapojua wanaonekana kwa kila wanachofanya, huwa wanaepuka kufanya mambo ya kizembe na ambayo yaniathiri biashara. Kwa kuweka kamera kwenye biashara yako, tena kwa gharama ambazo ni ndogo kabisa, utaondoa mianya mingi ya wizi na uzembe mwingine unaoathiri biashara yako.

Pata kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA uweze kujenga mfumo bora wa kuendesha biashara yako na kuondoa mianya ya wizi na uzembe. Wasiliana sasa na namba 0678977007 kupata nakala yako ya kitabu.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeyafafanua hayo vizuri na jinsi ya kuanza kuyafanyia kazi. Karibu ujifunze zaidi hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.