Tambua Uwezo Mkubwa Wa Akili Na Mwili Wako Na Jinsi Ya Kuutumia Kutenda Miujiza.
Rafiki yangu mpendwa,
Mtu aliyefariki dunia mwaka 1924 kama atafufuliwa na kurudi duniani mwaka 2024 ambayo ni miaka 100 tu imepita, atashangaa sana yale atakayoyaona. Hataamini kama hii ni dunia ambayo amewahi kuishi. Kwani vitu vingi atakavyokuwa anaviona, vitakuwa ni miujiza mikubwa kwake.
Kwamba watu wanaweza kuwasiliana wakiwa mabara mbalimbali huku wakionana! Kwamba watu wanaweza kwenda angani na kurudi duniani salama? Kwamba magonjwa mengi yaliyokuwa yanawasumbua watu kipindi hicho kwa sasa yana dawa. Hivi ni vitu ambavyo vitamshangaza sana, japo sisi tunaviona ni vitu vya kawaida kabisa.

Umekuwa unasikia habari za watu waliopokea miujiza mikubwa kwenye maisha yao. Wapo ambao wamepata uponyaji wa magonjwa ambayo waliambiwa hawawezi kupona. Wapo ambao wamenusurika kwenye ajali ambazo watu hawawezi kuelezea wamenusurikaje. Habari za wale ambao wamepokea miujiza mbalimbali kwenye maisha yao ni nyingi.
Swali ni je wewe umewahi kufanya au kupokea miujiza kwenye maisha yako? Je unajua unaweza kufanya miujiza mikubwa kwenye maisha yako? Na je unajua miujiza hiyo unaweza kuitengeneza mwenyewe na siyo mpaka usubiri wengine wakufanyie miujiza hiyo?
Haya ni maswali ambayo unakwenda kupata majibu yake kwenye kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.
Ni kweli kwamba una nguvu ya kutenda miujiza, ndiyo, wewe hapo unayo nguvu ndani yako ya kutenda miujiza kwenye maisha yako. Huhitaji kusubiri wengine wenye nguvu fulani ndiyo wakutendee miujiza, wala huhitaji kupata elimu fulani ndiyo uweze kutenda miujiza.
Kila binadamu aliye hai, ndani yake kuna uwezo mkubwa wa kutenda miujiza. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajui kama nguvu hizo ziko ndani yao, huku wale wachache ambao wamekuwa wanajua na kutumia nguvu hizo, wakiwa hawajui ni jinsi gani wamezipata, hivyo kushindwa kuwafundisha wengine jinsi ya kutenda miujiza pia.
Kwenye kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA unakwenda kujifunza nguvu kubwa iliyopo ndani yako ya kutenda miujiza, nguvu ambayo tayari unayo lakini umeiacha ikiwa imelala ndani yako. Kwa kujua uwepo wa nguvu hii na kuiamsha, utaweza kutenda miujiza mikubwa kwenye maisha yako.
Huenda huamini maelezo haya ninayokupa, huenda unajiambia siyo kweli kwamba kila mtu ana nguvu ya kutenda miujiza. Na utakuwa hujakosea kwa kutoamini haya, kwa sababu sisi binadamu huwa tunaamini vitu ambavyo tunaweza kuvitambua kwa milango mitano ya fahamu, yaani kuona, kusikia, kunusa, kuhisi na kuonja.
Lakini kuna vitu vingi tumekuwa tunaona madhara yake bila ya kupitia milango hiyo mitano ya fahamu. Mfano kama umewahi kuwasha televisheni au redio kwa kutumia rimoti, umegusa kifaa hicho ukiwa mbali, halafu tv au redio inawaka, je nini kimeipelekea kuwaka? Ni kwa sababu kuna nguvu usiyoiona, ambayo inatoka kwenye rimoti kwenda kwenye tv au redio na kuifanya iwake.
Chukua pia mfano wa simu, unawasiliana na aliye mbali, unaongea kwenye simu na kumsikia mtu akiongea, lakini mpo mbali, je sauti yako inapazwaje hewani mpaka kumfikia unayeongea naye? Sauti yako inageuzwa kuwa nguvu ambayo haionekani, inasafirishwa kwenye mawimbi na kufika kwenye simu ya yule unayeongea naye, kisha kubadilishwa na kuwa nguvu ambayo mtu anaweza kuisikia.
Kwa mifano hiyo michache, unaanza kupata mwanga kwamba dunia haiendeshwi na vitu unavyoweza kuving’amua kwa milango yako mitano ya fahamu pekee. Bali kuna nguvu nyingine ambazo huwezi kuzitambua kwa milango mitano ya fahamu, lakini madhara yake unaweza kuyaona.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye nguvu ya kutenda miujiza, tayari ipo ndani yako, lakini huwezi kuisikia, kuiona, kuionja, kuigusa au kuinusa. Nguvu hiyo imesambaa kwenye mwili wako na unaweza kuyaona madhara yake. Mfano pale unapopata tamaa ya kufanya mapenzi, unaweza kusukumwa kufanya chochote ili tu kutimiza tamaa hiyo. Hiyo ni nguvu ambayo iko ndani yako, ambayo ukiweza kuitumia vizuri itakuwezesha kufanya miujiza.
Kwenye kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA utakwenda kujifunza kuhusu nguvu ya miujiza iliyo ndani yako na jinsi unavyoweza kuitumia. Unakwenda kujifunza kuhusu ubongo wako ambao ndiyo kifaa muhimu kwenye mwili wako, ambacho ukiweza kukitumia vizuri utaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako. Utajifunza tabia za ubongo wenye furaha na jinsi ya kuzifikia ili kuzalisha furaha kwenye ubongo wako.
Baada ya kuujua mwili na ubongo wako, utakwenda kujifunza kuhusu vituo vya nguvu vilivyopo kwenye mwili wako na jinsi unavyoweza kukusanya nguvu za vituo hivyo na kuiunganisha na nguvu ya mawimbi inayoendesha dunia nzima na hapo kuweza kupata miujiza mikubwa.
Unachopaswa kujua ni kwamba nguvu ya miujiza tayari ipo ndani yako na tayari inakuzunguka hapo ulipo. Ili uweze kupoka miujiza yako ni lazima utambue nguvu zilizo kwenye mwili wako, uzikusanye na kuziunganisha na nguvu ya dunia. Yote hayo unakwenda kujifunza kwenye kitabu hiki.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha upate na kusoma kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, na kisha chukua hatua kwenye yale unayojifunza ili maisha yako yaweze kubadilika. Kupata kitabu hiki wasiliana na namba +255678977007 kwa siku, ujumbe au wasap na utapewa utaratibu wa kukipata kitabu popote ulipo.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimekushirikisha yaliyomo kwenye kitabu cha UNGA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA. Angalia kipindi hicho ili uone jinsi unavyokosa mengi kwa kutokutambua na kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.