Ni wazi kwamba, maamuzi mengi ya binadamu yanafanyika kwa hisia. Hasa pale anapoona kuna mazingira ya kukosa bidhaa husika.

Kuna utofauti kimaamuzi unafanyika pale unapoingia katika eneo la biashara na kuambiwa bidhaa hizi zimebakia chache au ofa ni leo tu. Pamoja na sehemu unayoambiwa bidhaa zipo za kutosha usiwe na wasiwasi.

Neno “zimebaki chache” kuna namna linafanya akili yako inawaza kwa haraka haraka jinsi ya kufanya ili kupata bidhaa au huduma husika.

Ikitokea pesa ipo kumudu gharama huwazi sana, unafanya malipo.

Hii ni tofauti na unapoambiwa bidhaa zipo, ni wewe tu kuamua unalipia lini.

Hapo akili inahisi uzito na haikupi sana ushirikiano katika kufanya maamuzi ya haraka.

Hii ni kwa sababu bidhaa zipo muda wote. Kama ni muuzaji mtabishana bei na maeneo mengine mengi.

Wakati mwingine unashawishika kutaka kujua bei za washindani wake.

Hivyo, katika ufuatiliaji unaofanya ni vema kuibua hali ya uharaka (Create a sense of urgency).

Waambie huduma hii tumekiweka ofa kwa ajili yako tu endapo ukilipia au ukianza leo. 

Faida za kutumia kanuni ya uhaba katika biashara;

Moja; Inaongeza hamasa .
Hapa mteja anahamasika kuchukua hatua za haraka, maana anahofia kukosa bidhaa husika. Biashara unayotumia kauli hii wanahamasika kuchukua hatua haraka.

Mbili; Inamfanya mteja kuwa karibu na biashara.
Hasa katika eneo la ufuatiliaji. Mteja anakuwa anafanya ufuatiliaji kuhusu ofa au bidhaa mpya ili asikose bidhaa.

Tatu; Inakuza mauzo
Hii ni kwa sababu wateja wa wanachukua hatua haraka kulipia.

Jinsi ya kutumia kanuni hii

Moja; Tumia ushuhuda
Waambie wateja juu ya waliochukua bidhaa husika hapo nyuma.

Mbili; Fanya kwa msimamo
Usitumie njia hii au kanuni ya uhaba mara moja ukaacha. Rejea mfano wa shule na vyuo.

Tatu; Ainisha manufaa anayopata mteja.
Manufaa haya yanaweza kuwa kwenye bei, usafiri au kitu kingine.

Kitu cha kuzingatia; Unapotumia kanuni ya uhaba, epuka kutaja idadi ya bidhaa. Ishia tu kusema zimebakia chache.

Mteja akiuliza bidhaa ngapi zimebakia? Muulize, kwa nini wewe unataka kiasi gani cha bidhaa au muda upi mzuri kuanza huduma?

Lengo ni kutojifunga kwenye mauzo.

Hatua za kuchukua leo; Angalia bidhaa unazoweza kuziingiza sokoni kama ofa na kuzitangaza. Wakati wa kuziuza ndipo unatumia uhaba. Lengo ni kukuza mauzo.

SOMA; Tumia Nguvu Ya Ofa Kuuza Bidhaa Zingine
Chukua hatua leo kukuza mauzo yako

Wako Wa Daima

Lackius Robert

Mkufunzi Wa Mauzo na Mwandishi

0767702659 / mkufunzi@mauzo.tz

Karibu tujifunze zaidi.