Rafiki yangu mpendwa,
Ukiwa hujafanikiwa, unayaona mafanikio ni magumu sana na yasiyowezekana katika hali ya kawaida.
Unaweza kuweka juhudi kubwa sana kwenye yale unayofanya, lakini bado matokeo yasije kama unavyokuwa unategemea.
Lakini baada ya kufanikiwa, ndiyo unashangaa jinsi ambavyo mafanikio yamekuwa rahisi. Na kufanikiwa zaidi inakuwa rahisi kwa sababu unakuwa umeshavuka kitu kikubwa kilichokuwa kinakuzuia.
Iko hivi rafiki, kabla hujafanikiwa, kikwazo kikubwa cha mafanikio huwa hakipo nje yako, bali kinaanzia ndani. Huwa kunakuwa na ukuta mwembamba sana kati yako na mafanikio makubwa unayotaka kufikia.
Lakini kwa bahati mbaya sana umekuwa huuoni ukuta huo na wala hujui jinsi ya kuuvuka ili kupata mafanikio unayoyataka.
Na kwa bahati mbaya sana, mafunzo mengi kuhusu mafanikio huwa hayafundishi kuhusu ukuta huo na jinsi ya kuuvunja. Mafunzo mengi huweka mkazo kwenye siri za mafanikio na vitu gani vya kufanya.

Watu wanajua yote hayo na wanafanya, lakini bado kuna kitu kinakuwa kinawazuia. Kukijua kitu hicho ni sawa na taa kuwashwa kwenye giza, kila kitu kinakuwa wazi kabisa.
Mimi rafiki yako nimejipa wajibu wa kuhakikisha wewe unajenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Hivyo kila wakati nimekuwa nafanya tafiti ni nini hasa kinakuzuia kupata mafanikio makubwa wakati unayataka na juhudi unaweka.
Kitu hiki kimoja ambacho nimekiona kwa wengi, kimekuwa kikwazo sana kwao kufanikiwa. Kwa hakika, ukiweza kuvuka kitu hicho kimoja, kutoboa inakuwa ni uhakika kwenye chochote unachofanya.
Rafiki, kwa uzito wa kitu hicho, sitaki tu ukisome, bali nataka unisikie nikiwa nakisema na kukusisitiza. Nataka kikuingie ndani ya moyo wako na mifupa yako ili kisikutoke kamwe. Kila mara ukikumbuke na kikusukume kufanya makubwa zaidi.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimekueleza kitu hicho kwa kina na hatua za kuchukua ili usikwamishwe tena na kitu hicho. Karibu ujifunze na kuchukua hatua ili uweze kupata mafanikio makubwa kwa uhakika.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.