3428; Kujisikia vizuri na kufanya vizuri.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Tunapotaka kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yetu, tunapaswa kuhangaika na mambo yanayofanya vizuri na siyo ya kujisikia vizuri.
Kujisikia vizuri huwa kunafurahisha, kwa sababu kunatimiza matakwa ya mtu ndani ya muda mfupi.
Lakini kujisikia vizuri huwa hakubadili maisha ya mtu.
Ni hisia za muda mfupi tu na huwa zinapita.
Mabadiliko ya kweli kwenye maisha yanatokana na yale mambo ambayo mtu unafanya.
Japo yanaweza yasionyeshe matokeo ya haraka, huwa yanaacha alama ya kudumu.
Kujisikia vizuri huwa kunasukumwa zaidi na wivu pale wengine wanapokuwa wanapiga hatua kubwa.
Huwa ni rahisi kuona kuna kitu hawafanyi kwa usahihi au kuna namna walisaidiwa kupiga hatua.
Kujisikia vizuri kwa kuwashusha chini wengine huwa hakuna matokeo zaidi ya hapo.
Na huo ndiyo ubaya wa kuendeshwa na hisia kwenye mamgo muhimu.
Mtu anaweza kujisikia vizuri sana, lakini hakuna hatua kubwa anazokuwa amepiga.
Weka mkazo wako kwenye kufanya vizuri na siyo kujisikia vizuri.
Matokeo ya kufanya yanadumu wakati yale hisia ni ya muda mfupi tu.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe