3429; Uhakika wa kushinda.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Kila ambacho mtu anafanya ni kwa sababu kuna matokeo fulani anayokuwa anategemea kuyapata.
Hivyo mtu anaweka malengo na mipango kwenye ufanyaji ili kuwa na uhakika wa matokeo atakayopata.

Licha ya hayo, bado matokeo ambayo wengi wamekuwa wanayapata ni tofauti kabisa na yale ambayo mtu alikuwa amedhamiria.
Kwa kifupi matokeo yanayokuwa yamepatikana yanakuwa ni tofauti kabisa na matarajio yaliyokuwepo.

Kama mtu anataka kupata matokeo mazuri kwa uhakika, kuna vitu anavyopaswa kuvipa uzito zaidi.

Pale mtu anapoweka lengo, anapaswa kuyaelekeza maisha yake yote kwenye kulifikia lengo hilo kwa uhakika.

Hiyo inamaanisha kwamba kila kitu ambacho mtu anafanya, kinalenga kumpa ushindi anaokuwa anautaka.
Tangu mtu anapokuwa ameamka, kila kitu anachojihusisha nacho kinahusika na kufikia lengo unalokuwa nalo.

Ni kupeleka umakini wako wote kwenye kitu kimoja kati ya vingi unavyojihusisha navyo na kukipa hicho kimoja kipaumbele zaidi ili kukifikia kwa uhakika.
Na kwa kuwa msingi wa umakini unafanya kazi, kila anayeweka umakini mkubwa kwenye kitu anachofanya, matokeo huwa ni ya uhakika.

Uhakika wa mafanikio yako uko ndani yako.
Kama kwa kuweka umakini wako wote kwenye kitu kimoja pekee kuna nguvu ya kupata matokeo mazuri, fikiria kama ukiyaelekeza maisha yako yote kwenye kujenga mafanikio makubwa.

Kwa hakika utaweza kupata kila unachotaka.
Peleka umakini wako wote kwenye malengo makubwa uliyonayo na hakuna namna utashindwa.
Ushindi kwako linakuwa ni swala la muda tu.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe