Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 41 na 42
Kwenye mbinu namba 41 tulijifunza ukamilishaji wa kuomba msamaha.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 42 tulijifunza ukamilishaji wa kukataa kuamini.
Na kwenye ukamilishaji wa kuomba msamaha, mbinu namba 41 tulijifunza kwamba pale unapokuwa umeshindwa kukamilisha mauzo kwa mara ya kwanza, unaomba msamaha kisha kutumia nafasi nyingine kukamilisha mauzo.
Na kwenye ukamilishaji wa kukataa kuamini, tulijifunza kwamba watu huwa hawawezi kufanya maamuzi peke yao, wanahitaji msaada. Hivyo pale mteja anaposhindwa kukamilisha mauzo, unamwambia kwamba bidhaa au huduma unayotoa ndicho kitu ambacho yeye anataka na ni sahihi kwake kuwa nacho.
Hivyo unamwambia kwamba hutaki kuamini kwamba hatakwenda kukamilisha mauzo kwa sababu ni bidhaa/huduma sahihi kwake na unajua anaitaka.
SOMA;Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 41-42
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 43 na 44.

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;
43. Ukamilishaji wa ndiyo tatu na basi.
Ndiyo ni neno lenye nguvu kubwa, muulize mteja maswali atakayojibu ndiyo kisha kamilisha mauzo.
Wala usimuulize kama atanunua au la, wewe chukulia kama tayari ameshakubali, kwa kujibu maswali yako ndiyo, nenda moja kwa moja kwenye kukamilisha.
Ndiyo zake zinakuwa zimemweka kwenye mwendo wa kukamilisha mauzo.
Acha ndiyo yake, imtenganishe na fedha zake mwenyewe.
Kwa mfano, unamwambia mteja hivi kwenye ukamilishaji huu;
“Je nimejibu maswali yako yote? Tumekuwa rahisi wewe kutufikia? Je mimi ni aina ya mtu unayetaka akuhudumie? Basi weka sahihi yako hapa, tukamilishe hili, tafadhali lipia bidhaa au huduma yako uende ukafurahie uwekezaji mzuri uliofanya leo.
44. Ukamilishaji wa rufaa.
Ukamilishaji huu unamfanya mteja aone ana nguvu ya majadiliano, kwa kukupa watu zaidi anaona atapata punguzo.
Pia watu wanapenda kuwasaidia wengine, wakiamini kwa kufanya hivyo na wao watasaidiwa.
Kwa mfano, unapokuwa na mteja na namna ya kukamilisha ukamilishaji huu, unamwambia mteja hivi;
“Kabla hatujaingia kwenye bei, nani mwingine unayemjua ambaye ana uhitaji wa bidhaa/huduma hii?”
Kitendo cha kumuuliza hilo swali, kisaikolojia tu tayari umeshachukulia yeye ameshakubali, kitendo cha kutoa rufaa na kukupa wewe muuzaji ni kiashiria kwamba amekubaliana na wewe na kilichobakia ni wewe tu kukamilisha mauzo.
Kuuza ni raha, kila mtu anapouza kuna raha fulani anaipata ndani yake. Kama mtu alikuwa hana shauku, tabasamu utaliona. Lakini kitendo cha kutokuuza kinakufanya ujisikie vibaya.
Kwa nini upitie yote hayo ya kujisikia vibaya wakati kuna mbinu za kuuza na mafunzo yote kutoka CHUO CHA MAUZO?
Muuzaji bora kuwahi kutokea, Ukamilishaji ni hatua ya mwisho ya lengo lolote ambalo mtu anakuwa anafanyia kazi. Ndiyo hatua inayoleta matokeo ambayo mtu anataka kupata.
Ukamilishaji siyo muhimu kwenye mauzo pekee, bali ni kwenye kila eneo la maisha. Hakuna kinachotokea mpaka mtu amepata kuungwa mkono na wengine kwenye kile anachotaka. Ukamilishaji ndiyo hatua ya kuungwa mkono kwenye jambo lolote lile. Na ukweli mchungu ni kwamba tofauti ya wanaofanikiwa na wasiofanikiwa inaanzia kwenye ukamilishaji. Wanaofanikiwa ni wale wanaoweza kukamilisha, kupata uungwaji mkono na watu sahihi kwenye jambo lao.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo.
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504