Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 49 na 50
Kwenye mbinu namba 49 tulijifunza ukamilishaji wa hakuna uhaba wa fedha
Na kwenye ukamilishaji wa namba 50 tulijifunza ukamilishaji wa sababu ya kununua.
Na kwenye ukamilishaji wa hakuna uhaba wa fedha, mbinu namba 49 tulijifunza kwamba huu ni ukamilishaji ambao unamkumbusha mteja kile kilicho muhimu zaidi.
Wakati fedha zinaweza kuzalishwa kwa wingi na hakuna uhaba, kuwa na furaha ndiyo kilicho muhimu zaidi.
Na kwenye ukamilishaji wa sababu ya kununua mbinu namba 50 tulijifunza kwamba unatumia ukamilishaji huu pale unapokutana na mteja mgumu ambaye anaendelea kutoa mapingamizi mapya kila unapojibu mapingamizi ya awali.
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 49-50
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 51na 52
Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

51. Ukamilishaji wa dakika za mwisho.
Unatumia ukamilishaji huu pale unapoona hakuna makubaliano yanayofikiwa. Unapaswa kuuliza mwishoni na siyo mwanzoni.
Kwa mfano, unamuuliza mteja hivi ;
“Ni bei gani itakayokufanya useme ndiyo kwenye haya manunuzi?”
Baada ya kumwambia hivyo, utapata makubaliano yanayofikiwa. Hivyo, utajua kama ni mteja anayetaka kununua au la.
52. Ukamilishaji wa kuhalalisha.
Ukamilishaji huu huwa unatumika kama majaribio ya kupima uwezo wa mtu kufanya maamuzi na kuhalalisha ni maamuzi sahihi kwake.
Unapokuwa na mteja, unamuuliza hivi;
“Unahalalishaje uwekezaji wa ukubwa huu?”
Baada ya kumwambia mteja hivyo, itakusaidia kupima uwezo wa mtu kufanya maamuzi na kuhalalisha ni maamuzi sahihi kwake au la.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504