Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 53 na 54
Kwenye mbinu namba 53 tulijifunza ukamilishaji wa kufunga
Na kwenye ukamilishaji wa namba 54 tulijifunza ukamilishaji wa kama niki…,je wewe uta…
Na kwenye ukamilishaji wa dakika za mwisho, mbinu namba 53 tulijifunza kwamba
Ukamilishaji huu unaibua mapingamizi yaliyofichwa na kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa hayatabadilika.
Ukamilishaji huu unamfungia mteja kwenye maamuzi aliyofanya na kumzuia asibadilike.
Na kwenye ukamilishaji wa kama niki…je wewe uta… mbinu namba 54 tulijifunza kwamba unatumia ukamilishaji huu mwishoni mwa mazungumzo na siyo mwanzoni. Hii ni kumweka mteja upande chanya, kama atakubali, unakuwa umekamilisha mauzo na kinachobaki ni kujibu mapingamizi yake.
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 53-54
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 55 na 56.

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;
- Ukamilishaji wa vitu vyote sawa.
Ukamilishaji huu unaondoa fedha kwenye majadiliano na kupata maamuzi ya mtu kwanza.
Kwa kuuliza kwa nini, utajua kwa kina jinsi mtu anavyofanya maamuzi, kitu kitakachokupa fursa ya kuweza kumshawishi.
Kwa mfano, unamwambia mteja hivi;
“Kama kila kitu kingekuwa sawa, ni bidhaa gani ungenunua na kwa nani?
Kwa nini? Kwa nini tena?” (Uliza kwa nini mpaka akose jibu).
Hapa unapaswa kumuuliza maswali mteja ya kwa nini mpaka akose jibu na kukubali kununua kile unachouza. Watu wanapokosa cha kujibu baada ya kumuuliza maswali mengi, mwisho anaishia kukubaliana na wewe.
Kukataa ataona ni kitu ambacho siyo sawa kwani atakuwa anajipinga yeye mwenyewe.
- Ukamilishaji wa fedha sawa.
Ukamilishaji huu ni kama uliopita, ila unaweka uzito kwa nani mteja yupo tayari kununua. Ukamilishaji huu unakusaidia kuibua mapingamizi yaliyofichika.
Kwa mfano, pale mteja anapokupa pingamizi fedha, unamwambia mteja hivi
“Kama fedha zingekuwa sawa, ni bidhaa gani ungenunua au ungekuwa tayari kununua kwa nani? Kwa nini? Kwa nini tena?” (Uliza kwa nini mpaka akose jibu).
Maswali ya kwa nini yatakusaidia kujua kama mteja anataka kweli kile unachouza au anakuzingua tu.
Biashara zinashindwa kwa sababu hazipati mapato ya kutosha kutokana na kutokukamilisha mauzo. Watu huweza kutoa sababu mbalimbali kwa nini biashara zinashindwa, lakini ya kwanza kabisa ni hiyo ya kushindwa kukamilisha mauzo na hata mipango mingine inayokuwepo.
Mwisho, Ukamilishaji ni hatua muhimu kwa kila mtu kupata kila anachotaka kwenye maisha yake.
Kwenye mazungumzo yoyote yale na mteja, hakikisha kuna kitu unakamalisha. Usikubali kutoka mikono mitupu, pambana kuhakikisha juhudi ulizoweka haziendi bure.
Kama umekosa mauzo, basi upate hata miadi, namba ya simu ya kuendelea kumfuatilia na mteja wa rufaa.
Kauli yetu inasema ABC-always be closing mara zote unapaswa kukamilisha wateja.
Nenda kakamilishe mauzo makubwa kadiri ya malengo yako uliyojiwekea leo.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504