Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,
Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya CHUO CHA MAUZO.
Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.
Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.
Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.
Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.
Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 55 na 56
Kwenye mbinu namba 55 tulijifunza ukamilishaji wa vitu vyote sawa.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 55 tulijifunza ukamilishaji huu unaondoa fedha kwenye majadiliano na kupata maamuzi ya mtu kwanza.
Na kwenye ukamilishaji wa fedha sawa, mbinu namba 56 tulijifunza kwamba Ukamilishaji huu ni kama uliopita, ila unaweka uzito kwa nani mteja yupo tayari kununua. Ukamilishaji huu unakusaidia kuibua mapingamizi yaliyofichika.
SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 55-56
Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 57 na 58
Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

- Ukamilishaji wa kutoa nakala.
Huu ni ukamilishaji wa ubobezi ambao unamfanya mteja aone amepata ushindi, kisha kuanza tena kukamilisha kitu ambacho wanakuwa hawajajiandaa nacho na hivyo kuwa rahisi kukubaliana na wewe.
Kwa mfano mteja anakuambia;
(Mteja anakuambia nipe nakala na nitaenda kufikiria.) “Nitafurahi sana kukupa nakala, nipe dakika moja nikakutolee nakala. (Unaenda kutoa nakala na kurudi),
Unamwambia,
Ndugu Mnunuaji, wakati natoa nakala nimefikiria kama bidhaa/huduma hii ingekuwa ndiyo kitu hasa unachotaka, kusingekuwa na haja ya kutoa nakala, ungefanya maamuzi kabisa. Nini hakijakaa sawa?”
- Ukamilishaji wa niachie makaratasi.
Ukamilishaji huu unamkumbusha mteja kwamba tayari ana majukumu mengi ya kufanya hivyo amalizane na hili mara moja badala ya kuendelea kujirundikia majukumu.
(Mteja anakuambia niachie makaratasi yenye maelezo na nitaenda kufikiria.) “Nitafurahi sana kukupa hayo makaratasi kama ningeona yanakusaidia, lakini nategemea mtu kama wewe umetingwa na mengi kwa sasa. Tufanye maamuzi sasa badala ya kukuongezea makaratasi mengi zaidi ya kufanyia kazi. Weka sahihi yako hapa, kinachofuata baada ya hapa ni wewe kukamilisha malipo, lipia sasa, ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo?
Mwisho, Ukamilishaji ni hatua muhimu kwa kila mtu kupata kila anachotaka kwenye maisha yake.
Kwenye mazungumzo yoyote yale na mteja, hakikisha kuna kitu unakamalisha. Usikubali kutoka mikono mitupu, pambana kuhakikisha juhudi ulizoweka haziendi bure.
Kama umekosa mauzo, basi upate hata miadi, namba ya simu ya kuendelea kumfuatilia na mteja wa rufaa.
Kauli yetu inasema ABC-always be closing mara zote unapaswa kukamilisha wateja.
Nenda kakamilishe mauzo makubwa kadiri ya malengo yako uliyojiwekea leo.
Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.
Shika kichwa chako na jiambie kauli hii; Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo
Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,
Mwl.Deogratius Kessy
Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504