Habari njema muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea,

Karibu sana kwenye mwendelezo wa makala zetu za ukamilishaji ambazo ni mwendelezo wa makala kutoka kwenye programu yetu ya  CHUO CHA MAUZO.

Hongera sana kwa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kwa haya unayoendelea kujifunza hapa.

Leo ni jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA.

Kama kauli mbiu inavyosema, mara zote unapaswa kukamilisha wateja na wewe pia unapaswa kukamilisha wateja. Na kukamilisha ndiyo wajibu wako namba moja kwenye biashara yako.
Wajibu wako namba moja ni kuuza na unapokuwa umemuuzia mteja maana yake umemkamilisha.
Hivyo basi, kila wakati wageuze wateja tarajiwa uliokuwa nao na waweze kununua na kuwa wateja kamili.

Ukamilishaji ndiyo kitu muhimu sana kwenye mauzo kwa sababu ndiyo kitu pekee kinacholeta fedha kwenye biashara kupitia kile unachouza iwe ni bidhaa au huduma.

Kwenye somo letu lililopita tulijifunza mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nayo ni mbinu namba 57 na 58

Kwenye mbinu namba 57 tulijifunza ukamilishaji wa vitu vyote sawa.
Na kwenye ukamilishaji wa namba 57 tulijifunza huu ni ukamilishaji wa ubobezi ambao unamfanya mteja aone amepata ushindi, kisha kuanza tena kukamilisha kitu ambacho wanakuwa hawajajiandaa nacho na hivyo kuwa rahisi kukubaliana na wewe.

Na kwenye ukamilishaji wa fedha sawa,  mbinu namba 58 tulijifunza kwamba Ukamilishaji huu unamkumbusha mteja kwamba tayari ana majukumu mengi ya kufanya hivyo amalizane na hili mara moja badala ya kuendelea kujirundikia majukumu.

SOMA; Mbinu Mbili Za Uhakika Za Ukamilishaji Wa Mauzo 57-58

Leo kwenye jumatano ya ukamilishaji tukiongozwa na kauli mbiu yetu inayosema ABC ALWAYS BE CLOSING-MARA ZOTE KUWA UNAKAMILISHA WATEJA, tunakwenda kujifunza mbinu nyingine mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo nazo ni mbinu namba 59 na 60.

Zifuatazo ni mbinu mbili za uhakika za ukamilishaji wa mauzo ambazo tunakwenda kujifunza hapa;

59. Ukamilishaji wa mtu muhimu.

Kwa mfano, unatumia mfano huu kwa mteja kumpa umuhimu wa hadhi ya juu;“Kwa sababu ya hadhi na ushawishi wako hapa mjini, tunakwenda kukupa ofa ambayo hatujawahi kumpa mtu mwingine yeyote. Weka sahihi yako hapa, tafadhali lipia, ipi njia nzuri kwako kukamilisha malipo?
Kamilisha malipo ili uende ukafurahie uwekezaji wako mzuri

Mara zote chukua muda wa kumtambua na kumthamini mteja, na pale unapokutana na mtu mwenye ushawishi na umaarufu, mwonyeshe unatambua na kuthamini hilo. Watu wanapenda sana kutambuliwa, kuthaminiwa na kuonekana ni wa muhimu. Ukionyesha hilo kwa watu utaweza kukamilisha mauzo zaidi.

60. Ukamilishaji wa mtu wa tatu.

Kwa mfano, unamwambia mteja hivi;

“Kama nikimshawishi muuzaji akakubaliana na hilo, je utakuwa tayari kukamilisha mauzo sasa? Weka sahihi yako hapa kisha nikaongee na muuzaji.”

Wewe kama muuzaji unakuwa kama mtu wa katikati, halafu kuna mteja anataka kununua, anataka kupunguziwa.
Sasa unamwambia kama nikienda kumshawishi, je, utakua tayari kununua sasa? Akisema ndiyo, tayari unamkamilisha.
Au wewe kama muuzaji unaweza kumwambia mteja kama nikienda kumshawishi meneja au bosi utakua tayari kununua? Akisema ndiyo unamkamilisha.

Unatumia ukamilishaji huu pale unapohitaji uthibitisho wa mtu mwingine kwenye mauzo. Kwa kuuliza hivyo, unamfanya mteja aone uko upande wake na hivyo kukubali kukamilisha mauzo.

Mwisho, Ukamilishaji ni hatua muhimu kwa kila mtu kupata kila anachotaka kwenye maisha yake.
Kwenye mazungumzo yoyote yale na mteja, hakikisha kuna kitu unakamalisha. Usikubali kutoka mikono mitupu, pambana kuhakikisha juhudi ulizoweka haziendi bure.
Kama umekosa mauzo, basi upate hata miadi, namba ya simu ya kuendelea kumfuatilia na mteja wa rufaa.

Kauli yetu inasema ABC-always be closing mara zote unapaswa kukamilisha wateja.
Nenda kakamilishe mauzo makubwa kadiri ya malengo yako uliyojiwekea leo.

Nenda leo ukawe mkamilishaji bora kabisa kuwahi kutokea na ukauze zaidi kupitia mbinu ulizojifunza leo na mbinu nyingine za nyuma ulizojifunza.

Shika kichwa chako na jiambie kauli hii;  Mimi … (Taja jina lako)
Ni muuzaji bora kuwahi kutokea.
Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo na leo ninakamilisha mauzo ya Tsh….Taja kiasi kwa kila mteja niliyemweka kwenye mchakato wa mauzo

Kutoka kwa muuzaji mwenzako, rafiki anayekupenda na kukujali,

Mwl.Deogratius Kessy

Mwalimu/Mwandishi/Mjasiriamali
Makamu Mkuu wa CHUO CHA MAUZO.
makamu@mauzo.tz, 📞0717101505//0767101504