
Rafiki Yangu Hivi Utajisikiaje Kama Ulikuwa Una Fursa Kujenga Utajiri Mkubwa Lakini Mwisho Unakufa Maskini?
Hakuna Kitu Ambacho Kinaniuma Kwenye Maisha Yangu Kama Mtu Huyu,
Anaamka Kila Siku Asubuhi anafanya Kazi Kwa Bidii na juhudi, Miaka 10, 20 , 30…
Anaamka Kila Siku Asubuhi Anakatisha Usingizi Wake Anaiacha Familia Yake,
Anafanya Kazi Kwenye Mazingira Hatarishi Anarudi Amechelewa Amechoka Sana,
Anarudi Analala Akiwa Amechoka.
Inakuwa Mzunguko ni Huo Huo Kwa mwaka, Kwa wiki, Kwa Siku.
Mwaka Kwa Mwaka, Wiki Kwa Wiki, Siku Kwa Siku,
Inafikia Sasa Mwili Umechoka Hauwezi Kufanya Kazi Tena,
Nguvu Zimeisha, Mbaya Zaidi Anakuwa Hana Uhuru Wa Kifedha,
Wakuweza Kuyaendesha Maisha Yake Anavyotaka Yeye.
Hili Linaniuma Sana, Kwasababu Naona Kabisa Lipo Ndani Ya Uwezo Wangu,
Na Ipo Ndani Ya Mtu Yeyote Kuweza Kujikwamua Kiuchumi,
Na Kufikia Uhuru Wa Kifedha Bila Ya Kujali Umejiajiri au Umeajiriwa,
Unafanya Vibarua au Vyovyote vile, Kama Tu Unayo Njia Ya Kuingiza Kipato Chochote Kile,
Basi Unao Uwezo Wa Uhakika Kabisa Wa Kujenga Utajiri na Kufikia Uhuru Wa Kifedha Kwenye Maisha Yako.
Hilo Linawezekana Kabisa Kwa Mtu Yeyote Yule Anayeingiza Kipato,
Kipato chochote Kile hata kama ni kidogo Sana,
Akiweza Kuwa na Nidhamu na Hicho Kipato Kidogo,
Kwa Miaka 1,2 3, 5 Mpaka Wa 30,
Lazima Atajenga Utajiri Mkubwa Sana,
Kwahiyo Tunaowatu Wengi Leo Hii Ambao hawajaweza Kujenga Utajiri Kwenye Maisha Yao.
KWANINI Tunao Watu Wengi Wa namna hiyo?
Kwa Sababu, Watu Wengi wanajizuia wao Wenyewe Kujenga Utajiri Mkubwa,
Matokeo Yake Sasa Wanaishia Kwenye Umaskini Wa Kutupwa,
Na Walikuwa Wanaouwezo Kabisa Wakujenga Utajiri Ndani Yao,
Fursa Zilikuwa Mbele Yao Lakini Wamejizuia Wao Wenyewe Kujenga huo Utajiri,
Na Leo Rafiki Yangu Ninaenda Kufungua Huko Kujifunga Ambako Unako,
Na Kama Utachukua hatua Nakuhakikishia Kwamba Muda Mrefu Utaweza Kujenga Utajiri Mkubwa.
Hiko Hivii Kujenga Utajiri Mkubwa Unahitaji Ngazi 5 Tu,!
- Ngazi Ya Kwanza ni Lazima Uwe na Kipato. Tayari Unacho. ndio maana Unasoma Hapa.
- Ngazi Ya Pili Lazima Udhibiti Matumizi Yako.
- Ngazi Ya Tatu Lazima Utoke Kwenye Madeni. Unaweza Ukawa Nayo na Yakakupa Shida.
- Ngazi Ya Nne Kuweka Akiba.
- Ngazi Ya Tano ni Kufanya Uwekezaji.
Ni Ngazi Tano Tu Ambazo Ukizifanyia Kazi Zinakupa Mafanikio Makubwa Kwa Mda Mrefu.
Lakini Unaweza Ukawa Unajua Kabisa,
…ni Lazima uingize kipato, udhibiti matumizi, Utoke Kwenye Madeni, uweke Akiba, na uwekeze,
Unakwama Wapi?
Rafiki Unajikwamisha Mwenyewe Kwa Kuruhusu Tabia Zako Binafsi, Hisia Zako, Saikolojia Yako, Mazoea Yako Kuingia katikati Yako na Utajiri Wako.
KWANINI Unaruhusu Tabia Zako, hisia Zako, Saikolojia Yako, Mazoea Yako Ziingie Katikati Yako?
Tunaenda Kuvunja Hizo Tabia Zinazokuzuia Kujenga Mafanikio Makubwa.
Tuje Kwenye mfano,
Zamani Kulikuwa Kuna Kodi ya Kichwa,
Wahenga Watakuwa Wanalijua Hili,
Huu Mchakato Wa Kodi Ya Kichwa,
Nakumbuka Nikiwa Bado Mdogo, Kijijini Walikuwa Wanakimbilia Mtoni,
Ili Tu Kukwepa Kulipa Kodi ya Kichwa,
Ulikuwa Unafwatwa Ulipe Kodi ya Kichwa, Ukikataa Kulipa Kodi,
Palepale Unakamatwa.
Baadae Watu Wakatumia Akili Kwanini Hawa Watu Tusumbuane Nao Kulipa Kodi ya Kichwa?
Tuwaambie Tu Kodi ya Kichwa Haipo, Tuiingize Pengine Lazima Watailipa,
Unajua Nini Kilitokea Waliitoa Kodi ya Kichwa,
Ikaja Kodi Ya Ongezo La Thamani
Ile Kodi Ambayo Uliambiwa Uiilipe Mwenyewe Unaponunua Kitu Chochote Unalipa Kodi Ndani Yake,
Sijui Unanielewa, Yaani Kwamba Ukiambiwa Ulipe Mwenyewe,
Kwahiari Yako Mwenyewe Utakimbia,
Na Hutaenda Kulipa Inaweza Kuwa Hela Ndogo Sana,
Lakini Inapowekwa Mahali Ambapo Unalipia Bila Kutaka.
Lazima Utailipa.
Mfano Wa Pili ni…
Kodi Ya Majengo
Aliyejenga Kipindi Cha Hivi Karibuni,
Atakuwa Anajua kwamba
Kuna tofauti Kubwa Sana Kati Ya Zamani na Sasa,
Kukusanya Kodi ya Majengo Ilikuwa ni Kazi Kubwa Sana Kwa serikali,
Kazi Nzito Sana, Ni Mpaka Watu Wapigiwe Kelele Sana,
Ilikuwa ni Fujo Sana ni Kuvutana Mashati….
Wakaangalia Huyu Mtu Anatumia Nini Kila Siku Wakagumdua Wanatumia Umeme Kila Siku,
Wakaingiza Kodi ya Jengo Kwenye Umeme, Inamaana Kwa Mwezi Ukinunua Umeme Kwa Mara ya Kwanza Wanalamba Kodi Yao Ya Jengo.
Na WanajuanHauwezi Kukataa Kulipa Umeme,
Kwahiyo Wanakusanya Kodi ya Umeme Bila Shida Yoyote Ile,
Kwasababu Hauwezi Kukaa Bila Kulipia Umeme, Unajikuta Unalipa Kodi ya Jengo Kupitia Umeme.
Rafiki Unaweza Ukawa unajionea Wewe Mwenyewe,
.
Unaona Kwamba Ukitaka Ufanye Kwa Hiari Yako Wewe Mwenyewe Utakwama,
Badala Yake Tafuta Kitu Ambacho Kitakufanya Ufanye Hata Kama SIYO Kwa Hiari Yako.
Yaani Kitakufanya Ufanye Moja Kwa Moja (Automatic).
Yaani SIYO Kwa Hiari Yako Ujisikie Kuweka Akiba (Automatic) Inakukata Moja Kwa Moja,
Kama Vile Unavyokatwa Kodi au Umeme.
…na Kwa Wale Ndugu Zetu Ambao Ukiambiwa Mshahara ni Milioni 1,
Hautakuja Kuishika Milioni 1 Kwa Mikono Yako Mwenyewe,
Utashangaa Imeingia milioni 8 Tu Ukiuliza Unaambiwa Umelipa Kodi.
Kwasababu Wanatambua Fika Kabisa,
Tabia Zako Zimeishinda Serikali,
Kwahiyo Kuivuka Hiyo
Unatakiwa Uweke Mfumo Ambao Utakao Kuwajibisha Kuweka Akiba,
…na Kuwekeza Moja Kwa Moja (Automatic)
Yaani Anza Kwa Kufungua Akaunti 3 Za Benki,
Akaunti Ya Kwanza Inakuwa Ni Kwaajili Ya Akiba,
Akaunti Ya Pili Inakuwa Ni Kwaajili Ya Uwekezaji.
Na Akaunti Ya Tatu Inakuwa Ni Ya Kwaajili Ya Malengo Maalum,
Sasa Baada Ya Hapo Nenda Kawaambie Benki Kila Tarehe Fulani ya Mwezi Husika Wakukate kiasi Fulani Kwenye Akaunti Yako Kuu Ya Kipato,
Iendee Kwenye Akaunti ya Akiba,
Nyingine Uwekezaji na Nyingine Malengo Maalum.
Alafu Wajibu Wako Mkuu ni Wewe Kuhakikisha Kila Baada ya Tarehe Husika unakuwa na Pesa Kwenye hiyo Akaunti,
Kisha Wanaikata Chapu.
Kwakufanya Hivi Utaondoa Ile Tabia Yako Inayokuzuia Kujenga Utajiri Mkubwa Kwenye Maisha Yako.
Lakini Ukitaka Utoboe Pekee Yako, Kwa Akili Yako, Kwa Tabia Zako Hizo, Kwa Hisia Zako, Kwa Mazoea Uliyonayo,
Rafiki Unajizuia Kufanikiwa.
Embu Fikiria Tu Serikali Imehangaika Kiasi Gani Mpaka Kujua Hawa Watu Lazima Wakatwe Juu Kwa Juu.
Fikiria Tena Kwenye Mifumo ya Mishahara Wanakata Moja Kwa Moja.
Kwasababu Akili Hatujiwezi.
Ondoka na Hili Rafiki, Nenda Katengeneze Mfumo Wa Kujikata Wewe mwenyewe Moja Kwa Moja.
Kama Kuna Watu Wanakulipa Unaweza Ukawapa Mpango Wako,
Kwamba Kila Unaponilipa Kiasi Fulani Niwekee Hapa Kwenye Mfumo Wangu Wa Uwekezaji.
…au Niwekee Pembeni Nitaichukua Baadae.
Fanya Hivyo, Kwasababu Ukikaa na FEDHA Mkononi Mashetani Yatakupanda,
Utashangaa Mara Imeisha.
Kwasababu Ya Mazoea na Tabia Ulizonazo,
Ambazo Zimekuwa ni Kikwazo Kwako Kujenga Utajiri Mkubwa,
Rafiki Kwahiyo Ondoka Hapa na Hili Somo,
Nenda Katengeneze Mfumo Unaokuwezesha Wewe Kujikata Pesa Moja Kwa Moja na kupeleka Kwenye Malengo Yako Uliyokuwa Nayo Mengine,
Usisubiri Uweze Kuweka Akiba Kwa utashi Wako Wewe Mwenyewe Lazima Utakwama.
Kumbuka Hii Ngoma ni Ya Miaka 10, 20, 30
Wengi Wanaanzaga na Mbio Kali Sana Mwanzoni,
Wiki za Kwanza Za Mwanzoni Mwezi Wa kwanza Baada ya Hapo Chali,
Kwasababu Tabia Zinarudi, Mazoea Yanarudi Anaishia Pale.
Wewe Kaa Mahali Ambapo
Itakusukuma na Kukufanya Uone Haibu Kuacha.
Kwasababu Mnaambatana na Kufanya, Hii Inakulazimisha Kwasababu Pekee Yako Utajidanganya,
Inabidi Ukae Kwenye Kundi Fulani,
Epuka Tabia Zako Kukuzuia Kufanikiwa,
Rafiki Kwa Kujiwekea mfumo Wa Moja Kwa Moja Kwenye Kuweka Akiba, Kuwekeza,
…na Kaa Kwenye Kundi Ambalo Litakusukuma Wewe Kufanya unachopaswa Kufanya.
…au Kuwa na Mtu Ambaye Anakusimamia Kwa Karibu.
Nakuhakikishia kwamba Utafanya Kweli Kwasababu Tabia Zako Zitakuzingua.
Lakini Ukiwa na Mtu Anayekusimamia,
Anahakikisha Unafanya na Utatoka Nje Ya Mazoea Yako,
…na Utaweza Kufanya Kwa Ukubwa Sana.
Nikukaribishe Rafiki Kwenye Program Ya NGUVU YA BUKU,
Huku Unapata Nguvu Ya Kundi Ya Wewe Kufanya Uwekezaji Kwa Muda Mrefu na Kuweza Kujenga Utajiri.
Hii ni Program Rahisi Sana Kwako,
Ni Kwa Shilingi Elfu Tu,
Utaweza Kujenga Utajiri Mkubwa Sana Kwenye Maisha Yako,
Anyway, Kupata Huduma Hii Bonyeza Hiyo Link Hapo Chini
KUMBUKA; Program Ya NGUVU YA BUKU, Bado ni Bure Kabisa.
Lakini Kiingilio ni Kitabu Cha MTAALA WA UTAJIRI.
Karibu Uungane na Wawekezaji Wenzako,
Yote Ni Hapa 👇
Karibu. 🙏