‎Mpendwa Rafiki,

‎Watu wengi wanaamini kuwa ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na hela nyingi ,milioni tano, kumi, au hata zaidi.

‎Wengine wanasema, Mimi ni wa mshahara wa chini, siwezi kufika mbali.

‎Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawajui kitu kimoja muhimu: nguvu ya buku moja tu.

‎Buku ambayo unaitumia bila mpango kila siku, inaweza kuwa tiketi yako ya kutoka kwenye umaskini hadi kwenye uhuru wa kifedha.

‎Ni mara ngapi umetumia buku kununua soda, chipsi, vocha, au kitu usichohitaji halafu ukaishia kusema, Ah ni buku tu?

‎Halafu mwisho wa mwezi unakuta umekopa, umeshindwa kuwekeza, hata akiba huna.

‎Inasikitisha, siyo? Sasa fikiria, kama kila siku unapoteza buku moja tu, ndani ya mwezi umepoteza buku 30.

‎Mwaka mzima? Hiyo ni buku  360,000!

‎Na kama ungezitumia kuanzisha biashara ndogo au kuwekeza, ungekuwa mbali.

‎Hiyo ndiyo nguvu tuliyo nayo lakini hatuitumii.

‎Wengi tulifundishwa kwamba hela nyingi ndiyo hujenga utajiri.

‎Tukaanza kusubiri mshahara mkubwa, *tende kubwa za kibiashara,” au *mjomba wa Dubai.*

‎Lakini hizo ni hadithi.

‎Angalia Uhalisia : Hela hujengeka kwa nidhamu na mpango, siyo kiasi.

‎Watu matajiri hawakuanza na mamilioni.

‎Walitumia kile kidogo walichokuwa nacho kwa akili.

‎Walitunza, wakawekeza, wakaendeleza.

‎Kwa hiyo, tukiachana na dhana ya nitakapoanza kupata hela kubwa, tunaweza kuanza safari ya utajiri hata leo,

‎ Kwa ile buku tuliyonayo mfukoni.

‎Sasa hebu tuweke wazi, unataka kujenga utajiri kwa kutumia buku?

‎Hizi hapa ni hatua 3 rahisi lakini zenye nguvu:

‎a. Weka akiba ya buku 1 kila siku:

‎Tafuta kopo, lipachike mahali salama. Kila siku, kabla ya kutumia hela yoyote, tengeneza tabia ya kuweka buku moja pembeni.

‎b. Anza kuwekeza kidogo:
‎Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na zaidi ya buku 30.

‎Tafuta biashara ndogo, lipia kozi fupi, au nunua bidhaa za kuuza mitandaoni.

‎c. Wekeza kwenye maarifa:

‎Buku moja inaweza kununua data. Tumia hiyo kusoma makala, kuangalia video za elimu ya fedha, au kusikiliza podcast. Maarifa ni mtaji.

‎Kuna jamaa yangu mmoja anaitwa Mussa,

‎Kabla hajajiunga na program ya NGUVU YA BUKU,

‎Alikuwa na mshahara wa laki na 20 kwa mwezi.

‎Alikuwa na majukumu mengi lakini alianza kuweka buku moja kila siku.

‎Miezi sita baadaye, alikuwa na buku 180.

‎ Akanunua kahawa na kuanza kuuza kikombe ofisini kwao, faida yake ilikuwa buku 2 kwa kila kikombe.

‎Siku moja akaniambia,

Bro, ile tabia ya kuweka buku moja kwa siku ilinibadilishia maisha. ‎ ‎Sasa hivi nina biashara mbili na bado naendelea kuweka akiba!

‎Ukweli ni huu:
‎Buku moja inaweza kuwa mtaji wa maisha yako mapya.

‎Usidharau kile kidogo, ndani yake kuna nguvu kubwa sana ya kifedha.

‎Anza leo, anza sasa.

‎Usisubiri mshahara mkubwa, anza na buku!

‎Ungependa kupata mwongozo wa kina wa jinsi ya kutumia nguvu ya buku kujenga utajiri?

‎Kupata Mwongozo Wa Kina Ingia Hapa 👇

https://wa.link/w4i6gb

‎Kumbuka; Buku yako ya leo, ndiyo utajiri wako wa kesho.

‎Karibu.
‎0756694090.