
Mpendwa Rafiki,
Hii Ndiyo Siri Ya Kuacha Kuishi Kwa Bahati Nasibu.
Kama umewahi kujiuliza, “Hivi mshahara wangu unaishia wapi?” au unashangaa kila mwezi hela yako inakatika bila hata kununua kitu kikubwa,
…basi hii makala ni yako. Watu wengi wanapambana na kitu kimoja, kutokujua kutumia na kusimamia pesa zao binafsi kwa mpangilio.
Na matokeo yake, kila mwezi unakuwa kama sinema ile ile ya huzuni.
Hebu fikiria… unafanya kazi kama punda, unapata mshahara au kipato fulani, lakini mwisho wa mwezi unaomba mpaka nauli.
Akiba huna, mikopo unayo, na kila hela ikija ni kama upepo unapuliza.
Hali kama hii inavunja moyo. Inakufanya uanze kuamini kuwa labda “mimi sina bahati na pesa,” kumbe tatizo si pesa,
…ni usimamizi wako.
Watu wengi huamini kwamba ili uweze kujiwekea akiba au kupanga matumizi yako, lazima uwe na kipato kikubwa.
Uongo mtupu.
Hakuna hela ndogo, kuna matumizi mabaya.
Hata ukiwa unapata elfu kumi kwa siku, ukiwa na mpango, unaweza kuweka akiba, ukawekeza, na ukaishi kwa amani bila presha.
Tatizo ni kuishi bila bajeti, kutumia kwa mazoea, na kuiga maisha ya watu mitandaoni.
Sasa sikiliza: Suluhisho la kweli ni kujifunza kusimamia kipato chako kwa nidhamu.
Andika mapato na matumizi.
Tengeneza bajeti ya wiki au mwezi.
Anza kuweka akiba kila unachopata – hata kama ni buku kwa siku.
Epuka matumizi yasiyo na tija, kama vile vinywaji, usafiri wa kifahari, au mlo wa kila siku unaoweza kupunguzwa.
Jifunze pia kuwekeza kidogo, hata kwenye maarifa kama vitabu au kozi za fedha.
Usimamizi wa fedha sio ugumu ni maamuzi.
Nakumbuka mshikaji wangu Sule kutoka Tabata.
Alikuwa anapata mshahara wa laki tatu, lakini alikuwa hana akiba hata ya elfu tano.
Nilimshauri aanze kutumia app ya kufuatilia matumizi yake, na kila siku aweke buku moja kwenye bahasha ya akiba.
Mwaka mmoja tu baadaye, alikuwa ameweka zaidi ya laki tatu na nusu, akajifunza kupitia kozi ya NGUVU YA BUKU, na leo ana ka-biashara ka kuuza vocha na bidhaa za mtandaoni.
Sasa ananiambia, “Bro, kumbe shida yangu haikuwa mshahara, ilikuwa nidhamu.”
Sasa ni wakati wako.
Anza kuzitawala fedha zako.
Jifunze kusimamia fedha zako mwenyewe.
Hatua ndogo leo, ni uhuru mkubwa kesho.
Kama ungependa kujifunza zaidi kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na kupata tools kali kama app, vitabu na kozi.
Basi Bonyeza Hapa:
👉 https://wa.link/pxqntw
Au piga: 0756 694 090
Karibu Tujenge Maisha Bila Presha.
Imeandikwa Na Bwana Ramadhan Amir