‎Mpendwa Rafiki,
‎
‎Hii Ndiyo Siri Ya Kuacha Kuishi Kwa Bahati Nasibu.
‎
‎Kama umewahi kujiuliza, “Hivi mshahara wangu unaishia wapi?” au unashangaa kila mwezi hela yako inakatika bila hata kununua kitu kikubwa,
‎
‎…basi hii makala ni yako. Watu wengi wanapambana na kitu kimoja, kutokujua kutumia na kusimamia pesa zao binafsi kwa mpangilio.
‎
‎Na matokeo yake, kila mwezi unakuwa kama sinema ile ile ya huzuni.
‎
‎Hebu fikiria… unafanya kazi kama punda, unapata mshahara au kipato fulani, lakini mwisho wa mwezi unaomba mpaka nauli.
‎
‎Akiba huna, mikopo unayo, na kila hela ikija ni kama upepo unapuliza.
‎
‎Hali kama hii inavunja moyo. Inakufanya uanze kuamini kuwa labda “mimi sina bahati na pesa,” kumbe tatizo si pesa,
‎
‎…ni usimamizi wako.
‎
‎Watu wengi huamini kwamba ili uweze kujiwekea akiba au kupanga matumizi yako, lazima uwe na kipato kikubwa.
‎
‎ Uongo mtupu.
‎
‎Hakuna hela ndogo, kuna matumizi mabaya.
‎
‎Hata ukiwa unapata elfu kumi kwa siku, ukiwa na mpango, unaweza kuweka akiba, ukawekeza, na ukaishi kwa amani bila presha.
‎
‎Tatizo ni kuishi bila bajeti, kutumia kwa mazoea, na kuiga maisha ya watu mitandaoni.
‎
‎Sasa sikiliza: Suluhisho la kweli ni kujifunza kusimamia kipato chako kwa nidhamu.
‎
‎Andika mapato na matumizi.
‎
‎Tengeneza bajeti ya wiki au mwezi.
‎
‎Anza kuweka akiba kila unachopata – hata kama ni buku kwa siku.
‎
‎Epuka matumizi yasiyo na tija, kama vile vinywaji, usafiri wa kifahari, au mlo wa kila siku unaoweza kupunguzwa.
‎
‎Jifunze pia kuwekeza kidogo, hata kwenye maarifa kama vitabu au kozi za fedha.
‎
‎ Usimamizi wa fedha sio ugumu ni maamuzi.
‎
‎Nakumbuka mshikaji wangu Sule kutoka Tabata.
‎
‎Alikuwa anapata mshahara wa laki tatu, lakini alikuwa hana akiba hata ya elfu tano.
‎
‎Nilimshauri aanze kutumia app ya kufuatilia matumizi yake, na kila siku aweke buku moja kwenye bahasha ya akiba.
‎
‎Mwaka mmoja tu baadaye, alikuwa ameweka zaidi ya laki tatu na nusu, akajifunza kupitia kozi ya NGUVU YA BUKU, na leo ana ka-biashara ka kuuza vocha na bidhaa za mtandaoni.
‎
‎Sasa ananiambia, “Bro, kumbe shida yangu haikuwa mshahara, ilikuwa nidhamu.”
‎
‎Sasa ni wakati wako.
‎
‎Anza kuzitawala fedha zako.
‎
‎Jifunze kusimamia fedha zako mwenyewe.
‎
‎Hatua ndogo leo, ni uhuru mkubwa kesho.
‎
‎Kama ungependa kujifunza zaidi kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na kupata tools kali kama app, vitabu na kozi.
‎
‎Basi Bonyeza  Hapa:
‎
‎👉 https://wa.link/pxqntw
‎
‎Au piga: 0756 694 090
‎
‎Karibu Tujenge Maisha Bila Presha.

Imeandikwa Na Bwana Ramadhan Amir
‎
‎