Kakaa/Dadaa Yangu….

‎💥 Unajua shida ya wengi?
‎Wengi wanaanza biashara kwa kishindo…
‎Lakini baada ya miezi mitatu,
‎BAM! Kimya kama kaburi la usiku.

‎Wanaanza kuuza nguo,
‎Wanaingiza mzigo wa milioni mbili,
‎Lakini hakuna anayenunua.
‎Wanashindwa kuelewa nini kinakwenda kombo.

‎Wanakata tamaa fasta.
‎Wanarejea kutegemea mshahara.
‎Wengine wanakata tamaa kabisa—wanakufa na ndoto zao.

‎💔 Na hapa ndipo kuna maumivu makali.
‎Biashara si kupost tu bidhaa kwenye status.
‎Si kutegemea rafiki zako watanunua.

‎Wala si kushusha bei kila siku eti “promo.”
‎Ukiwa huna akili ya mjasiriamali mjanja
‎utachezewa kama karata mitaani.

‎🎯 Ngoja nikufunze kitu.
‎Mjasiriamali mjanja ana akili ya pesa.
‎Anajua kutafuta wateja wake popote.
‎Anajua jinsi ya kuwashawishi bila kusumbua.

‎Anajua kutoa ofa ambayo haiwezi kukataliwa.
‎Anaelewa psychology ya mteja.
‎Na zaidi ya yote, anajua kuji-brand.

‎Na kama hujui hayo yote,
‎Usijidanganye eti “ni mapenzi ya Mungu.”
‎Ni mapenzi ya kukosa maarifa.

‎⚙️ Sasa suluhisho liko hivi:
‎Ukiamua kuwa mjanja kwenye biashara
‎Lazima ujue kuuza hadithi.

‎Ndiyo, HADITHI!
‎Watu wananunua stori kabla ya bidhaa.
‎Wakiigusa hadithi yako,
‎Wanafika mwisho wa status tayari wamejishawishi.

‎Ukiuza sabuni,
‎Usiuze sabuni uza usafi wa mtoto wao.
‎Ukiuza viatu,

‎Usiuze kiatu uza heshima ya mguu wake kazini.
‎Mjasiriamali mjanja anauza HISIA si bidhaa tu.

‎🧠 Nikupe hadithi moja ya kweli.

‎Mrembo mmoja anaitwa Amina.
‎Alikuwa anauza mikoba Kariakoo.
‎Alihangaika sana, kila siku status 50, likes 2, wateja 0.

‎Alipojifunza kuuza kwa stori, mambo yalianza kubadilika.
‎Siku moja aliandika:

‎“Mwanamke mmoja alikuja dukani kwangu, akiwa amechoka, alinyamaza muda mrefu…

‎Aliponunua hii handbag,

‎alisema, ‘Kwa mara ya kwanza najihisi mwanamke kamili.’

‎Niliogopa kusema chochote,
‎ila moyo wangu ulichanua.
‎Na hapo ndipo nilijua,
‎Siuzi mikoba, nauza imani kwa mwanamke.”

‎Dakika 20 baadaye mikoba 7 iliuzwa.

‎🔥 Sasa uliza tena… MJASIRIAMALI MJANJA ni nani?



‎Ni yule anayejifunza kila siku.
‎Anayefikiria tofauti.
‎Anayejua kutumia lugha ya wateja.
‎Anayeuza kwa hisia, si bei.

‎Wewe je?
‎Upo kwenye biashara kwa bahati,
‎au umeamua kuwa MJASIRIAMALI MJANJA?

‎😎 Kumbuka hii ya mwisho:
‎Wakati wengine wanauza bidhaa,
‎MJANJA ANAUZA STORI INAYOCHOMA MOYO.

‎MUHIMU; Kama bado hujasoma kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA,

‎Ukweli ni kwamba unajipunja,

‎Kukipata Piga Simu 0756694090.

‎Karibu.
‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.