
Rafiki Yangu….
Alichopenda zaidi ilikuwa pipi. Kila aliponunuliwa pipi, alikuwa na furaha.
Lakini alipokua, pipi zikageuka kuwa simu, viatu vya bei, na maisha ya kuigiza kwenye mitandao.
Kitu kimoja hakikubadilika alikuwa bado hajui thamani ya pesa.
Mama yake alimsomesha shule nzuri.
Lakini hakumfundisha elimu ya fedha.
Makala hii itakuonyesha kwa nini ni muhimu kuanza kufundisha watoto elimu ya fedha wakiwa bado wadogo na jinsi unavyoweza kuanza leo, hata kama wewe si mtaalamu wa pesa.
Mwanao anaweza kuwa mtoto wa tofauti.
Anajua kuweka akiba.
Anaelewa thamani ya kazi.
Anaweza kupanga matumizi yake mwenyewe.
Anaweza kuanzisha biashara ya kuwauzia watoto wenzake vitu vya shule.
Ana mwelekeo wa kuwa huru kifedha kabla ya miaka 25.
Na yote yanaanzia na mafunzo madogo unayompa leo.
Wazazi wengi wanaanza kufundisha watoto wao masuala ya fedha wakiwa na miaka 6 tu.
Na matokeo ni ya kushangaza.
Mtoto wa miaka 10 ana bajeti yake.
Mtoto wa miaka 13 ana akaunti ya akiba.
Mtoto wa miaka 15 tayari anauza bidhaa mtandaoni.
Si kwa sababu ni “kwa bahati.” Ni kwa sababu walifundishwa.
Elimu ya fedha kwa mtoto wako haimaanishi kumpeleka darasani.
Inaanza kwa hatua ndogo kama hizi:
Mfundishe kutofautisha “nataka” na “nahitaji.”
Mpe fedha kidogo, mfundishe kuigawa kwenye matumizi, akiba, na msaada.
Mpe changamoto ya kuweka akiba kwa lengo maalum (kama kununua toy au kitabu).
Mshirikishe kwenye maamuzi madogo ya kifamilia kuhusu fedha.
Mpatie hadithi za watoto kuhusu pesa (vitabu, video, au michezo).
Unachofanya hapa ni kumjengea msingi wa maisha ya kiuchumi yenye busara.
Usisubiri mtoto akue ili uanze kumfundisha fedha.
Anajifunza kwa kukuangalia sasa.
Na kila siku inayopita bila elimu hii ni siku ya hasara kwa maisha yake ya baadaye.
Chukua hatua leo:
Anza kwa mazungumzo madogo, mifano midogo, na maamuzi madogo.
Kwa sababu kesho ya mtoto wako inajengwa leo.
Usimwachie dunia imfundishe mwanao kuhusu fedha maana dunia hufundisha kwa uchungu.
Fursa ni yako.
Wakati ni sasa.
Mfundishe pesa, kabla pesa haijamfundisha yeye.
Anway, kama bado hujathibitisha ushiriki wa uzinduzi wa program ya Nguvu Ya Buku Toto.
Imebaki Siku Ya Leo Tu!
Yaani ndio siku ya mwisho.
Kwahiyo wahi nafasi yako Sasa,
Kwa Kutuma Ujumbe NATAKA NGUVU YA BUKU TOTO
Kwenda 0756694090.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan