
Rafiki yangu,
Watu wengi wanapenda mafanikio…
Lakini wachache wako tayari kulipa thamani yake.
Wanataka maisha mazuri, pesa nyingi, heshima, uhuru…
Lakini wanataka yote hayo bila kutoa kitu cha thamani.
Huu ndio ukweli mchungu:
Kila mafanikio makubwa yana thamani fulani uliyoitoa.
Si uchawi, si bahati.
Ni gharama.
Na si lazima iwe pesa inaweza kuwa muda, nidhamu, maumivu, kujifunza, au hata kukataliwa.
Watu Wanapenda Matokeo, Sio Safari
Tazama watu wengi mitaani.
Wanakataa kulala masaa machache, kusoma, lakini wanataka UTAJIRI.
Wanataka kufungua biashara, lakini wakipata changamoto ya kwanza wanakata tamaa wanaacha.
Wanataka kuwa bora, lakini hawako tayari kupitia maumivu ya ukuaji.
Wanataka matunda bila kupanda mbegu.
Na hapo ndipo ndoto nyingi hufia njiani.
Mafanikio Hayaji Kwa Bahati
Ukiwaona waliopiga hatua kubwa, usidhani walibahatika.
Wamelipa bei kimya kimya.
Walilala wakiwa wanapanga, walipoamka walichukua hatua.
Wengine walikataliwa, wakachekwa, wakasahauliwa,
Lakini hawakukata tamaa.
Walijua kitu kimoja muhimu sana:
Kuna thamani lazima utoe kabla ya mafanikio kuonekana.
Tatizo ni kwamba, wengi wanadanganywa na mitandao.
Wanamuona mtu amefanikiwa, wanadhani ni short cut.
Hawajui nyuma yake kuna machozi, kukatishwa tamaa, majaribu, na bidii isiyo na mwisho.
Ndiyo maana leo unaona watu wanachoka mapema.
Wanakata tamaa haraka, kwa sababu hawakujua mafanikio ni vita, si zawadi.
Unalipa Kabla Ya Kupokea
Rafiki yangu, hakuna kitu cha bure duniani.
Kila mafanikio unayoyaona, kuna mtu amelipa gharama yake.
Mwanafunzi anayeongoza darasani, amelipa kwa kusoma usiku.
Mjasiriamali anayeuza sana, amelipa kwa kujaribu mara nyingi bila kukata tamaa.
Mtu mwenye utulivu wa akili amelipa kwa kuacha mambo yasiyo na maana.
Swali ni Je! Wewe upo tayari kulipa nini kwa mafanikio unayotaka?
Suluhisho Sio Bahati Ni Thamani Unayotoa
Unataka mafanikio ya kweli?
Anza kutoa thamani kwanza.
Toa zaidi ya unachotarajia kupokea.
Saidia watu.
Jifunze.
Kua mwaminifu.
Fanya kazi kwa bidii hata kama hakuna anayekuona.
Mafanikio ni matokeo ya kile unachotoa, sio cha kile unachotamani.
Namkumbuka kijana mmoja niliyezungumza naye mwaka jana.
Aliniambia, Kaka Ramadhani, nimechoka. Nimefanya biashara miezi sita bila mafanikio.
Nikamuuliza swali moja tu:
Ni thamani gani umetoa kwa wateja wako hadi sasa?
Akanyamaza.
Alikuwa anauza, lakini hakuwa anasaidia.
Anapost, lakini hajengi uhusiano.
Anaomba watu wanunue, lakini hawajui kwa nini wanapaswa kufanya hivyo.
Tulianza kufanyia kazi sehemu moja tu kujenga thamani kabla ya kuuza.
Baada ya miezi mitatu, alianza kupokea wateja wapya kila wiki.
Leo ananiambia, Kaka, sasa najua mafanikio ni matokeo ya thamani niliyojenga, si bidhaa nilizonazo.
Hakuna mafanikio bila gharama.
Kila unachotamani, kina bei yake.
Na kadri unavyotoa thamani zaidi, ndivyo mafanikio yako yanavyokukaribia haraka.
Usiogope kutoa.
Usiogope kusubiri.
Usiogope kulipa gharama.
Kwa sababu gharama ni mlango wa mafanikio yako ya kudumu.
Ukitaka kuelewa kwa kina kanuni za kweli za mafanikio,
na kujua namna ya kujenga maisha yenye thamani, mafanikio, na utulivu wa ndani,
Soma kitabu hiki kipya kinachotikisa watu wengi,
FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO
Ndani yake utajifunza:
Siri ya watu wanaofanikiwa kimya kimya
Kwa nini wengine hukwama hata wakiwa na juhudi
Namna ya kulipa thamani sahihi bila kuumia
Na jinsi ya kuishi maisha yenye kusudi, heshima, na utajiri wa kweli.
Usiache siku ipite bila kusoma kitabu hiki.
Kwa sababu wakati wengine wanasubiri bahati,
watu wachache wanajifunza jinsi ya kujenga mafanikio kwa kutoa thamani.
Pata nakala yako ya FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO sasa:
Kwa kubonyeza hapa 👇
👉 https://wa.link/eqqp80
Karibu.
0756 694 090
PS: Jenga thamani, mafanikio yatakufuata.