‎Rafiki yangu,
‎Watu wengi wanapenda mafanikio…
‎Lakini wachache wako tayari kulipa thamani yake.
‎
‎Wanataka maisha mazuri, pesa nyingi, heshima, uhuru…
‎Lakini wanataka yote hayo bila kutoa kitu cha thamani.
‎
‎Huu ndio ukweli mchungu:
‎Kila mafanikio makubwa yana thamani fulani uliyoitoa.
‎
‎Si uchawi, si bahati.
‎Ni gharama.
‎Na si lazima iwe pesa inaweza kuwa muda, nidhamu, maumivu, kujifunza, au hata kukataliwa.
‎
‎ Watu Wanapenda Matokeo, Sio Safari
‎
‎Tazama watu wengi mitaani.
‎Wanakataa kulala masaa machache, kusoma, lakini wanataka UTAJIRI.
‎Wanataka kufungua biashara, lakini wakipata changamoto ya kwanza wanakata tamaa wanaacha.
‎
‎Wanataka kuwa bora, lakini hawako tayari kupitia maumivu ya ukuaji.
‎
‎Wanataka matunda bila kupanda mbegu.
‎Na hapo ndipo ndoto nyingi hufia njiani.
‎
‎Mafanikio Hayaji Kwa Bahati
‎
‎Ukiwaona waliopiga hatua kubwa, usidhani walibahatika.
‎Wamelipa bei kimya kimya.
‎Walilala wakiwa wanapanga, walipoamka walichukua hatua.
‎
‎Wengine walikataliwa, wakachekwa, wakasahauliwa,
‎Lakini hawakukata tamaa.
‎
‎Walijua kitu kimoja muhimu sana:
‎Kuna thamani lazima utoe kabla ya mafanikio kuonekana.
‎
‎Tatizo ni kwamba, wengi wanadanganywa na mitandao.
‎Wanamuona mtu amefanikiwa, wanadhani ni short cut.
‎
‎Hawajui nyuma yake kuna machozi, kukatishwa tamaa, majaribu, na bidii isiyo na mwisho.
‎
‎Ndiyo maana leo unaona watu wanachoka mapema.
‎Wanakata tamaa haraka, kwa sababu hawakujua mafanikio ni vita, si zawadi.
‎
‎Unalipa Kabla Ya Kupokea
‎
‎Rafiki yangu, hakuna kitu cha bure duniani.
‎Kila mafanikio unayoyaona, kuna mtu amelipa gharama yake.
‎
‎Mwanafunzi anayeongoza darasani, amelipa kwa kusoma usiku.
‎Mjasiriamali anayeuza sana, amelipa kwa kujaribu mara nyingi bila kukata tamaa.
‎
‎Mtu mwenye utulivu wa akili amelipa kwa kuacha mambo yasiyo na maana.
‎
‎Swali ni Je! Wewe upo tayari kulipa nini kwa mafanikio unayotaka?
‎
‎Suluhisho Sio Bahati Ni Thamani Unayotoa
‎
‎Unataka mafanikio ya kweli?
‎Anza kutoa thamani kwanza.
‎Toa zaidi ya unachotarajia kupokea.
‎
‎Saidia watu.
‎Jifunze.
‎Kua mwaminifu.
‎Fanya kazi kwa bidii hata kama hakuna anayekuona.
‎
‎Mafanikio ni matokeo ya kile unachotoa, sio cha kile unachotamani.
‎
‎Namkumbuka kijana mmoja niliyezungumza naye mwaka jana.
‎Aliniambia, Kaka Ramadhani, nimechoka. Nimefanya biashara miezi sita bila mafanikio.
‎
‎Nikamuuliza swali moja tu:
‎Ni thamani gani umetoa kwa wateja wako hadi sasa?
‎
‎Akanyamaza.
‎Alikuwa anauza, lakini hakuwa anasaidia.
‎
‎Anapost, lakini hajengi uhusiano.
‎Anaomba watu wanunue, lakini hawajui kwa nini wanapaswa kufanya hivyo.
‎
‎Tulianza kufanyia kazi sehemu moja tu kujenga thamani kabla ya kuuza.
‎Baada ya miezi mitatu, alianza kupokea wateja wapya kila wiki.
‎
‎Leo ananiambia, Kaka, sasa najua mafanikio ni matokeo ya thamani niliyojenga, si bidhaa nilizonazo.
‎
‎Hakuna mafanikio bila gharama.
‎Kila unachotamani, kina bei yake.
‎Na kadri unavyotoa thamani zaidi, ndivyo mafanikio yako yanavyokukaribia haraka.
‎
‎Usiogope kutoa.
‎Usiogope kusubiri.
‎Usiogope kulipa gharama.
‎
‎Kwa sababu gharama ni mlango wa mafanikio yako ya kudumu.
‎
‎Ukitaka kuelewa kwa kina kanuni za kweli za mafanikio,
‎na kujua namna ya kujenga maisha yenye thamani, mafanikio, na utulivu wa ndani,
‎
‎Soma kitabu hiki kipya kinachotikisa watu wengi,
‎
‎FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO
‎
‎Ndani yake utajifunza:
‎
‎Siri ya watu wanaofanikiwa kimya kimya
‎
‎Kwa nini wengine hukwama hata wakiwa na juhudi
‎
‎Namna ya kulipa thamani sahihi bila kuumia
‎
‎Na jinsi ya kuishi maisha yenye kusudi, heshima, na utajiri wa kweli.
‎
‎Usiache siku ipite bila kusoma kitabu hiki.
‎Kwa sababu wakati wengine wanasubiri bahati,
‎watu wachache wanajifunza jinsi ya kujenga mafanikio kwa kutoa thamani.
‎
‎Pata nakala yako ya FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO sasa:
‎
‎Kwa kubonyeza hapa 👇
‎👉 https://wa.link/eqqp80
‎
‎Karibu.
‎ 0756 694 090
‎
‎PS: Jenga thamani, mafanikio yatakufuata.
‎