
Rafiki Yangu,
Kuna wakati maisha yanakupiga ngumi usiyoitarajia.
Unapoteza kazi.
Unasalitiwa.
Unakataliwa.
Unajitahidi lakini matokeo huyaoni.
Na hapo ndipo wengi hukata tamaa.
Wengine hukaa na kulia usiku kucha.
Wanajiona wameshindwa.
Wanahisi dunia imewaacha nyuma.
Lakini hebu nikuulize swali moja, rafiki…
Je, kulia kunabadilisha kitu?
Je, machozi yamewahi kulipa kodi?
Je, huzuni imewahi kuandika ukurasa mpya wa maisha yako?
Watu wengi hawajui kwamba maumivu si adui ni mwalimu.
Tatizo ni kwamba wengi wanashindwa kutafsiri somo lake.
Wanalia badala ya kusikiliza.
Wanajilaumu badala ya kujifunza.
Wanajificha badala ya kujijenga.
Hapo ndipo tofauti inapoanzia kati ya waliolia na waliotumia akili.
Waliolia walipoteza nguvu.
Lakini waliotumia akili walitawala maumivu yao, wakayageuza kuwa mafuta ya kusukuma maisha mapya.
Unajua kinachouma zaidi?
Ni pale unaona mtu ambaye mmepitia maumivu yanayofanana,
…lakini yeye ameyatumia kupanda juu,
na wewe bado upo hapo hapo,
…na unajiuliza Kwa nini mimi?
Ni kama dunia inakuonyesha picha ya vile ungepaswa kuwa,
…kama tu ungeamua kuamka badala ya kulia.
Kama tu ungeamua kutumia akili badala ya hasira.
Kama tu ungeamua kuona fursa badala ya huzuni.
Maumivu si hukumu. Ni changamoto.
Swali ni utayatawala, au yatakutawala?
Usidanganyike na maneno ya mitaani..
Eti subiri tu, bahati yako itafika.
Hapana!
Hakuna bahati inayofika bila akili kufanya kazi.
Hakuna maumivu yanayopotea kama hujayatawala.
Na hakuna mafanikio bila nidhamu ya kiakili.
Watu wanaofanikiwa sio wale wasio na maumivu,
…bali ni wale wanaotumia akili kuyageuza kuwa nguvu.
Hivyo acha kusubiri huruma.
Haitaokoa maisha yako.
Kitu pekee kitakachokutoa hapo ulipo ni mtazamo mpya wa kiakili.
Ukijua namna ya kutawala maumivu yako unakuwa na nguvu ya ajabu.
Unaanza kuona mbali.
Unaanza kujenga mipango mipya.
Unaanza kuvutia mafanikio, kwa sababu akili yako imezoea kusimamia hisia zako.
Kila tatizo linakuwa kama gym.
Kila changamoto inakuimarisha misuli ya ndani.
Ndipo unagundua:
Maumivu sio mwisho ni mwanzo wa toleo jipya la wewe bora zaidi.
Nakumbuka kijana mmoja aliwahi kuniambia,
Kaka Ramadhan, nilipoteza kila kitu. Biashara, mpenzi, na hata marafiki.
Nilimtazama na kumuuliza, Na baada ya hapo ulifanya nini?” Akanijibu kwa tabasamu: Nilikaa chini, nikaandika maumivu yangu kama ramani.
Nilijifunza kosa lilikuwa wapi.
Nikaweka akili yangu kufanya kazi siyo kulalamika.
Leo, maumivu yale ndiyo yamenifanya niwe mtu ninayeongoza timu yangu,
na ninasaidia wengine kujijenga tena.*
Nilijua pale maumivu yakitawaliwa, yanazaa nguvu mpya.
Rafiki yangu,
acha kutumia machozi kama silaha.
Yatumie kama maji ya kupunguza moto wa hasira ndani yako.
Wakati wengine wanalia,
wewe kaa kimya tafakari.
Chukua somo, jifunze, geuza huzuni yako kuwa ngazi ya kupanda juu.
Usikubali maumivu yakutawale.
Yatawale kwa akili.
Tumia falsafa ya ustoa kujitawala kwanza, kabla ya kuutawala ulimwengu.
Soma kitabu hiki kipya cha
FALSAFA YA USTOA, Ili ujitawale Mwenyewe, kisha Uitawale Dunia.
Kitabu hiki ndio ramani ya kujenga akili imara, moyo thabiti, na maisha yasiyotetereka.
Usikimbie maumivu yajue, yashinde, uyatumie.
👉 Sasa ni zamu yako kutawala maumivu yako kabla hayajakutawala wewe.
Unakipata hapa 👇 kwa ofa
https://wa.link/524kl0
Karibu.
0756694090.