‎Rafiki Yangu,
‎
‎Kuna kipindi unajikuta unaumia sana…
‎Si mwili, bali moyo.
‎Umeamini mtu, akakusaliti.
‎
‎Umejitahidi, ukaanguka.
‎Umeweka juhudi, matokeo hayaji.
‎Na hapo ndipo wengi hukosea, wanaruhusu maumivu yawatawale.
‎
‎Wanakuwa wagumu, wanajifungia, wanakata tamaa.
‎Wanajidanganya kwamba sina tena bahati, au labda si mimi.
‎
‎Lakini ukweli ni huu maumivu si adui wako, ni mwalimu wako.
‎Yanakuja kukuonyesha sehemu unayopaswa kukua.
‎
‎Kila maumivu yana ujumbe.
‎Yanakuambia, hapo ulikuwa hujajua,
‎Yanakuambia, hapo unahitaji kubadilika.
‎Lakini wengi wanayakimbia badala ya kuyasikiliza.
‎
‎Unapokimbia maumivu, unajinyima maarifa.
‎Unapokubali kukaa nayo, unaanza kujijua.
‎Unagundua nguvu zako halisi zipo ndani sio nje.
‎
‎Sasa ngoja nikuambie kitu cha kweli kabisa…
‎Hakuna mtu aliyefanikiwa bila kuumia.
‎Kila mtu aliyejenga mafanikio makubwa, aliwahi kulia usiku mmoja.
‎Lakini hawakulia bure. Walilia, kisha wakajifunza.
‎
‎Na wakatoka wakiwa wamesoma somo ambalo vitabu havifundishi, somo la maisha.
‎
‎Nilimkuta kijana mmoja Arusha, alikuwa na duka dogo la nguo.
‎Akaibiwa mzigo wake wote usiku mmoja.
‎
‎Wiki nzima alikuwa amepotea, hana raha.
‎Nilipokutana naye, nikamwambia, Usiruhusu maumivu haya yakutawale yafanye yakufundishe.
‎
‎Akanitazama akaniambia, Lakini nimeumia sana.
‎Nikajibu, “Ndiyo, ila ndani ya maumivu hayo kuna siri ya mwelekeo mpya.*
‎
‎Baada ya miezi mitatu, akafungua duka jipya, safari hii akaweka mfumo wa usalama, akaanza kuuza online.
‎
‎Leo, ananiambia, Kama nisingeibiwa, nisingejua kuwa nilikuwa najibana.
‎
‎Hapo ndipo nilielewa kabisa, maumivu ni zawadi iliyofungwa kwa karatasi ya mateso.
‎
‎Ni somo linalokuandaa kuwa toleo jipya la wewe bora zaidi.
‎
‎Kama kuna kitu kimekukwaza leo, usikimbie.
‎Kaa nacho, uliza somo lake ni lipi.
‎
‎Maisha hayakupi adhabu, yanakupa mafunzo.
‎Tatizo ni sisi, tunatazama maumivu kwa macho ya huzuni badala ya macho ya uelewa.
‎
‎Wacha maumivu yakufundishe nidhamu, ujasiri, na upendo wa kweli.
‎
‎Lakini kamwe usiyape ruhusa yakutawale, maana yakikutawala yanafunga milango ya fursa zako.
‎
‎Unapojifunza kuvumilia, unaanza kuelewa falsafa ya ndani ya ustoa.
‎Ustoa ni kujitawala.
‎Ni kuamua kwamba mimi si rahisi kuvunjika.
‎
‎Ni kuelewa kwamba dunia haina huruma, lakini wewe unaweza kujitawala ili uishi kwa amani ndani ya machungu.
‎
‎Watu wengi leo wanaishi wakiwa mateka wa yaliyopita.
‎Wamefungwa na majeraha ya zamani.
‎Wanabeba hasira, chuki, na majuto.
‎
‎Lakini mtu mwenye hekima anajua: kupona ni uamuzi, si bahati.
‎Uamuzi wa kusema, Sitanung’unika tena, nitajifunza.
‎
‎Kila wakati unapojikuta umepigwa chini, kumbuka sio mwisho wako, ni mwanzo wa somo jipya.
‎
‎Maumivu yanakutaka utoke pale ulipo.
‎Yanataka uamke.
‎Yanataka ukubali kuwa safari ya ukuaji haianzi na furaha, huanza na maumivu.
‎
‎Wacha yakufundishe uvumilivu, nidhamu, na ustahimilivu.
‎Lakini usiyape nguvu ya kukuongoza, maana yakikupata, yanakufanya uwe mwepesi kukata tamaa, kulalamika, na kulaumu.
‎
‎Wewe sio mwathirika, wewe ni mwanafunzi wa maisha.
‎
‎Na kama unataka kujifunza zaidi namna ya kujitawala, kuishi kwa amani hata katikati ya maumivu, basi soma kitabu FALSAFA YA USTOA.
‎
‎Ndani yake utajifunza namna ya kutawala hisia zako, kupunguza machungu, na kuendelea mbele ukiwa na utulivu wa ndani.
‎
‎Kama unataka kuishi maisha ambayo maumivu yanakuwa walimu wako, sio mabwana wako,
‎
‎… basi kitabu hiki ni cha lazima kwako.
‎
‎Wacha maumivu yakufundishe, usiyape ruhusa yakutawale.
‎
‎Soma FALSAFA YA USTOA leo, na jifunze sanaa ya kujitawala ili uitawale dunia.
‎
‎Hiki hapa 👇
‎
‎https://wa.link/524kl0
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎