
Rafiki Yangu,
Kuna watu wengi sana wanafanya kazi usiku na mchana, lakini bado fedha inawakimbia.
Unapata mshahara leo, ndani ya siku 15 huna hata mia mfukoni.
Unajiuliza, Hivi pesa yangu inaenda wapi?
Siri ni moja tu fedha imekukataa.
Umeifanya adui yako bila kujua.
Sasa ngoja nikuambie kitu ambacho shule haikukufundisha…
Fedha ni kama rafiki mzuri.
Inahitaji utunzaji, heshima, na mpangilio.
Ukijua jinsi ya kuishi nayo vizuri, itakupenda.
Ukiona pesa kama kitu cha kuipoteza haraka, itakutoroka haraka zaidi.
Wengi tunalalamika hatuna pesa, lakini ukweli ni kwamba hatujui kuishi na pesa.
Tunaitumia vibaya, tunaitisha mkopo kwa hasira, tunanunua vitu vya kuonyesha, si vya kutengeneza.
Tunapanga kutumia kesho, lakini hatupangi kuwekeza leo.
Ndiyo maana kila mwezi unarudia historia ileile unapata, unatumia, unalalamika.
Lakini hebu fikiria hivi…
Kama ungeanza kuitazama fedha kama rafiki, ungefanyaje?
Rafiki unampangia muda, unamjali, unamfahamu tabia zake.
Hivyo ndivyo unavyotakiwa kufanya na fedha.
Unapaswa kuijua tabia yake.
Fedha inampenda mtu anayejua kuipanga.
Inampenda mtu anayejua kuizalisha.
Inampenda mtu anayejua kuiheshimu.
Hii hapa siri:
Usitumie fedha yako yote.
Anza na buku moja, iweke pembeni kila siku.
Tengeneza tabia ya kuwekeza hata kidogo, lakini kwa uthabiti.
Fedha ikiona unaiamini, inaanza kukuamini pia.
Inaongezeka polepole hadi unashangaa kumbe siri ilikuwa nidhamu tu!
Ninajua unafikiri huwezi kuwekeza kwa kipato chako cha sasa.
Lakini ukweli ni huu, hakuna kipato kidogo kwa mtu mwenye akili kubwa.
Tatizo si kiasi cha pesa, ni namna unavyoitazama.
Wengine walianza kwa elfu moja, leo wana biashara zinazowalipa milioni.
Walianza tu wakati wengine walikuwa wanasubiri mshahara mkubwa.
Nikupe mfano wa kweli kabisa…
Kuna jamaa mmoja aliyeamua kujiwekea buku moja kila siku.
Kila siku, bila kukosa.
Miaka miwili baadaye, alianza biashara ndogo ya kuuza juisi.
Leo ana kiwanda kidogo cha vinywaji, na anasema jambo moja tu:
Nilipoanza kuiheshimu pesa, ndipo pesa ilipoanza kuniheshimu mimi.
Ndugu yangu,
Fedha si adui yako.
Ni silaha yako ya uhuru, lakini kama huijui, itakupiga wewe.
Ukitaka kuishi maisha ya amani ya kifedha, jifunze kuifanya pesa iwe rafiki yako.
Anza kuwekeza, jifunze misingi ya fedha, jenga tabia mpya leo.
Na kama unataka kujua jinsi ya kulala huku pesa zako zikikufanyia kazi,
Basi soma kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA UWEKEZAJI.
Kitakufundisha namna ya kujenga urafiki wa kweli na fedha.
Urafiki utakaokufanya uitawale, badala ya kukutawala.
Bonyeza hapa 👇 kukipata kwa ofa,
https://wa.link/kj1hrl
Karibu.
0756694090.
PS: Fedha Ni Rafiki Mzuri Sana…
Lakini Ni Adui Mbaya Usipomuelewa.