Hii Ndio Siri Ya Watu Wenye Utulivu Wa Ajabu!
‎
‎Watu Wachache Wanaijua, Lakini Inawafanya Waishi Maisha Yasiyotikisika
‎
‎Rafiki Yangu,
‎
‎Kuna watu wanapitia changamoto kubwa…
‎Lakini bado wanatabasamu.
‎Hawakimbii.
‎Hawapigi kelele.
‎Wanakaa kimya, wanatulia, wanatafakari.
‎
‎Unashangaa, Anawezaje kuwa mtulivu wakati mambo yameharibika hivi?
‎
‎Wakati wengine wanapoteza mwelekeo,
‎wengine wanabaki imara kama mwamba.
‎
‎Siri yao ni moja tu..
‎ Wamejifunza kutawala akili zao.
‎Si kwa sababu maisha yao ni rahisi
‎bali wameamua kuwa watulivu hata wakati dunia inawapigia kelele.
‎
‎Utulivu hauji kwa bahati.
‎Ni maamuzi ya ndani.
‎Ni nidhamu ya akili.
‎Ni ujuzi wa kujitawala.
‎
‎Lakini wengi wanashindwa hilo.
‎Wanakasirika haraka.
‎Wanachoka mapema.
‎Wanavunjika moyo kwa jambo dogo.
‎Wanakuwa watumwa wa hisia zao.
‎
‎Kuna watu wanaamka na furaha asubuhi,
‎lakini saa tatu tu wanakuwa wameshajaa hasira.
‎Kila kitu kinawakasirisha.
‎Kila mtu anawaudhi.
‎
‎Na mwisho wa siku,
‎wanajiona wamechoka, wamepotea, wamevunjika ndani.
‎
‎Maisha yao ni kama redio yenye kelele.
‎Hawatulii.
‎Hawana amani.
‎
‎Hiyo ndiyo sababu watu wengi hawafiki walikopanga.
‎Sio kwa sababu hawana maarifa,
‎bali kwa sababu hawajui utulivu wa ndani unavyofanya akili ifanye kazi vizuri.
‎
‎Usidanganywe na mawazo ya mitaani.
‎Eti mtu mtulivu ni dhaifu.
‎Eti kukaa kimya ni kuogopa.
‎Hapana!
‎
‎Utulivu ni nguvu.
‎Kimya ni silaha.
‎Mtu mwenye utulivu anaona mbali kuliko wenye kelele.
‎
‎Watu wengi wanadhani nguvu ni kupiga kelele,
‎kuonesha hasira, au kushindana na kila mtu.
‎Lakini ukweli ni kwamba…
‎nguvu ya kweli ni kujua lini usiseme kitu.
‎Ni kujua namna ya kufikiri kabla ya kutenda.
‎
‎Mtu mwenye utulivu hajali nani anamchokoza.
‎Anajua thamani ya amani yake ya ndani.
‎
‎Sasa hebu jiulize,
‎unawezaje kuwa na utulivu huo wa ajabu?
‎
‎Kwanza, anza kujijua.
‎Tambua kinachokukasirisha, kinachokuvunja moyo, kinachokukengeusha.
‎Ukishakijua, unakimilikisha.
‎
‎Pili, jifunze kukaa kimya.
‎Wakati unahisi unataka kujibu haraka kaa kimya.
‎Wakati unahisi unataka kulipiza kisasi tulia.
‎Hapo ndipo nguvu inaanza kukua.
‎
‎Tatu, fanya maamuzi ukiwa umetulia.
‎Hasira, huzuni, au hofu hazina uwezo wa kuona mbali.
‎Lakini akili iliyotulia inaona fursa hata katikati ya giza.
‎
‎Utulivu ni kama macho ya ndani.
‎Unapoona wazi, unaishi vizuri.
‎
‎Namkumbuka rafiki yangu mmoja, Said,
‎alikuwa anapoteza mteja mkubwa kila alipokasirika.
‎Kila mara akihisi kudharauliwa, anajibu kwa ukali.
‎Na mwisho wa siku, anajikuta ameharibu dili.
‎
‎Siku moja aliniambia,
‎Bro Rama, nimechoka kuharibu kila kitu kwa hasira zangu.
‎
‎Tukakaa, nikamfundisha kitu kimoja…
‎Tulia kwanza. Hasira zikipita, ndipo utajua cha kusema.
‎
‎Akanisikiliza.
‎Miezi michache baadaye, akanipigia simu.
‎“Bro, kile ulichoniambia kimeniokoa.
‎
‎Nilipotulia, niliweza kusaini mkataba ambao nilikuwa nakaribia kuharibu.
‎Sasa najua, utulivu ni nguvu kuliko maneno.
‎
‎Leo, Said ni mmoja wa watu wanaoheshimika kazini kwake.
‎Watu wanamwambia, Bro, una utulivu wa ajabu!
‎
‎Anacheka tu, anajua siri yake ni moja alijifunza kujitawala.
‎
‎Rafiki yangu,
‎usitafute utulivu kwa kutoroka matatizo.
‎Tafuta utulivu kwa kujijua.
‎Kwa kuutawala moyo wako.
‎Kwa kuamua kuwa imara hata wakati mambo ni magumu.
‎
‎Hiyo ndio siri ya watu wenye utulivu wa ajabu.
‎Wamejifunza kwamba nguvu ya kweli haiko kwenye misuli,
‎bali iko kwenye akili tulivu.
‎
‎Kwa sababu mtu mwenye utulivu wa ndani,
‎anaweza kushinda vita yoyote ya nje.
‎
‎Anyway kujifunza zaidi,
‎
‎Soma kitabu hiki kipya cha
‎FALSAFA YA USTOA
‎
‎Kitabu hiki kinakufundisha siri ya kutawala akili yako,
‎kutuliza moyo wako,
‎na kuishi maisha yenye amani hata katikati ya kelele za dunia.
‎
‎Kupata kitabu hiki bonyeza hapa 👇
‎
‎https://wa.link/524kl0
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎
‎PS: Utulivu Ni Nguvu. Jifunze Kuimiliki Leo.
‎