Sikiliza hapa;

Rafiki yangu mpendwa,

Kila mtu anayeingiza kipato, anao uwezo wa kujenga utajiri. Haijalishi kiasi cha kipato ambacho mtu anaingiza, kama tu anaweza kuwa na matumizi yasiyozidi kipato hicho, anakuwa na ziada. Akiweka akiba na kuwekeza ziada hiyo, anaweza kujenga utajiri, kutegemea muda na aina ya uwekezaji atakaofanya.

Kiasi cha utajiri ambao mtu anaweza kujenga, kinategemea sana ukubwa wa kipato anachoingiza na matumizi anayokuwa nayo. Kadiri mtu anavyokuwa na kipato kikubwa na matumizi madogo, ndivyo anavyoweza kujenga utajiri mkubwa.

Ukubwa wa kipato ambacho mtu anaweza kuingiza, unategemea jinsi anavyolipwa. Kuna njia mbalimbali za kulipwa, na baadhi ya njia hizo zina ukomo wa kiasi cha kipato ambacho mtu anaweza kuingiza.

Kwenye hii #BaruaYaKocha tunaenda kuangalia njia mbalimbali za kulipwa na jinsi zinavyoathiri kiasi cha utajiri ambao mtu unaweza kujenga. Lengo la barua hii ni ujitafakari na kujua upo kwenye njia zipi na zipi njia sahihi kwako kuwa.

1. Kulipwa baada ya kufanya kazi.

Hii ndiyo njia iliyozoeleka kwa wengi, ambapo mtu anafanya kazi kwanza kisha ndiyo analipwa. Wafanyakazi wanaolipwa mishahara wapo kwenye njia hii, ambapo wanafanya kazi kwa kipindi husika kisha ndiyo wanalipwa.

Watu wanaofanya kazi za muda, za usaidizi na za kutumia nguvu, nao pia wapo kwenye njia hii. Watafanya kazi kwanza, kisha ndiyo watapata malipo waliyoahidiwa.

Kuna watu wapo kwenye biashara ambao nao wanatumia njia hii. Wanawapa wateja bidhaa au huduma kwanza, kisha wanategemea kulipwa baadaye.

Njia hii imekuwa inaonekana ni rahisi na wengi wanaitumia, lakini ni njia ya chini na yenye ukomo mkubwa kwa mtu kujenga utajiri.

Changamoto kubwa ya njia hii ni ukomo wa kulipwa. Kwa sababu malipo yanategemea mtu afanye kazi au kutoa bidhaa/huduma kwa mtu, kunakuwa na ukomo wa muda na nguvu za kufanya kazi au biashara husika.

Changamoto nyingine, ambayo ni hatari kubwa ya njia hii ni kutokulipwa. Japo mtu anakuwa ameahidiwa kulipwa baada ya kazi, wapo ambao hujikuta hawalipwi kabisa au kucheleweshewa malipo. Wapo wafanyakazi wanaocheleweshewa mishahara, pia wafanyabiashara wanaokopesha na kutokulipwa.

Hii haipaswi kuwa njia pekee na tegemeo kwa mtu kujenga utajiri mkubwa. Inaweza kuwa njia ya kuanzia, lakini mtu anapaswa kuitumia kama ngazi ya kwenda kwenye njia nyingine.

2. Kulipwa kabla ya kufanya kazi.

Wapo watu wanaotoka kwenye njia ya kulipwa baada ya kufanya kazi na kuweza kujitengenezea njia ya kulipwa kwanza ndipo wafanye kazi. Kwa njia hii, mtu anakuwa ameshajihakikishia malipo kabla hata hajafanya kazi. Na mara nyingi, malipo yanaweza kuwa makubwa kuliko ya wale ambao wanalipwa baada ya kufanya kazi.

Njia hii inatumiwa sana na wataalamu wanaouza huduma zao za kitaalamu kwa kulipwa kwanza kisha kutoa huduma. Kwa biashara ni zile ambazo wateja wanalipa kwanza ndiyo wanapata bidhaa au huduma.

Mtu aliyeajiriwa, ambaye analipwa mshahara baada ya kufanya kazi, anaweza kutumia utaalamu na uzoefu wake kutoa huduma za ushauri elekezi kwa kulipwa kwanza kabla ya kufanya kazi. Anachofanya ni kile kile, lakini anakuwa amebadili anakifanya kwa watu gani.

Changamoto ya njia hii ni ukomo wa muda wa kufanya kazi. Japo mtu analipwa kabla ya kazi, lakini analazimika kufanya kazi. Iwe atafanya yeye au watafanya watu, kunakuwa na ukomo wa kiasi gani mtu anaweza kulipwa. Hata kwa biashara zinazouza kwa wateja kulipa kabla, zinakuwa na ukomo.

Pamoja na njia hii kutokuwa na hatari ya kutokulipwa, bado inakuwa na hatari ya kukosa walipaji wengi. Kwenye jamii na uchumi ambao watu wamezoea kulipa baada ya kupata wanachotaka, anayetaka kulipwa kabla anaweza asipate wateja wengi.

Endelea kusoma #BaruaYaKocha hapa; #BZK128; Jinsi Unavyolipwa Inaamua Kiasi Cha Utajiri Unaoweza Kujenga