
Karibu kwenye huduma maalumu ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI inayoitwa STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA.
Huduma hii inawalenga wale ambao wanataka kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yao ili kuishi maisha wanayoyataka, bila kulazimika kufanya kazi moja kwa moja.
Kwenye huduma hii utapewa mwongozo wa kukokotoa kiasi cha uwekezaji unachopaswa kuwa nacho kwenye umri ambao umechagua kustaafu ambacho kitakuwezesha kumudu gharama za maisha yako bila kulazimika kufanya kazi moja kwa moja.
Kisha unasaidiwa kuweka mpango wa kukuwezesha kuwa na kiasi hicho cha uwekezaji kwa kujua kiasi cha kuwekeza kila mwezi.
Utaongozwa kuweka mipango sahihi kwenye maeneo yote ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI ambapo ni kuongeza KIPATO, kudhibiti MATUMIZI, kuondoka kwenye MADENI na kuweka AKIBA NA KUWEKEZA.
Kwenye huduma hii utapata usimamizi wa karibu kwenye kutekeleza mipango yote ya USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI ili uweze kufikia uhuru wa kifedha kwenye muda uliopanga.
JINSI PROGRAMU INAVYOFANYA KAZI.
Programu hii ya STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA inafanya kazi kwa mpango ufuatao;
1. Unaanza na umri ulionao sasa na umri ambao unataka uwe umefikia uhuru wa kifedha. Mfano kwa sasa una miaka 40 na unataka uwe umefikia uhuru wa kifedha ukiwa na miaka 60. Hapo una tofauti ya miaka 20.
2. Unakadiria gharama za maisha yako pale unapokuwa umefikia uhuru wa kifedha, yaani hiyo miaka 20 ijayo. Kwa kutumia kanuni maalumu inayopatikana kwenye programu hii, utajua kiasi sahihi kwa kuzingatia mfumuko wa bei kulingana na muda.
3. Ukishajua kiasi unachohitaji kuendesha gharama za maisha ukiwa umefikia uhuru wa kifedha, unakokotoa uwekezaji unaohitaji kuwa nao ili ukitoa asilimia 4 kwa mwaka itoshe kuendesha maisha yako. Asilimia 4 kwa mwaka ni kiasi cha uwekezaji wako ambacho ukitumia hutaweza kumaliza uwekezaji huo kwa kipindi chote cha maisha yako. Hivyo hata kama hufanyi kazi kabisa, bado una uhakika wa maisha mpaka unakufa, kama tu hutatumia zaidi ya asilimia 4 ya uwekezaji wako kwa mwaka.
4. Ukishajua kiasi cha uwekezaji unachopaswa kuwa nacho wakati umefikia uhuru wa kifedha, kuna kanuni maalumu ya programu hii ambayo utaitumia kukokotoa kiasi unachopaswa kuanza kuwekeza sasa ili kwa huo muda uliobaki nao uweze kufikia hicho kiwango cha uwekezaji.
5. Hapo sasa unawekwa mpango kamili ambao utaufanyia kazi, kuanzia kiasi cha kuongeza kwenye KIPATO, udhibiti wa MATUMIZI, kutoka kwenye MADENI yanayokugharimu na KUWEKEZA kila mwezi bila kuacha. Utaongozwa na kusimamiwa kwa karibu kwenye hayo maeneo yote mpaka ufikie lengo la uhuru wa kifedha.
Hii ni programu ambayo ukiifanyia kazi, matokeo yake yatakuwa ya uhakika kabisa bila ya kujali unaanzia wapi kwa sasa.
VIGEZO VYA HUDUMA
Ili kupata huduma hii ya STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA, unapaswa kukidhi vigezo hivi vitatu, vyote kwa pamoja;
1. Una kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI kilichoandikwa na Kocha Dr. Makirita Amani.
2. Una akaunti ya uwekezaji UTT na tayari umeshaanza kuwekeza.
3. Una uwezo na utayari wa kulipa ada ya huduma ambayo ni asilimia 10 ya kiasi unachowekeza kila mwezi (Kiasi cha chini Tsh 10,000/= na kiasi cha juu Tsh 100,000/=. Yaani kama unafanya uwekezaji mkubwa sana, ada ya juu kabisa utakayolipa ni laki moja kwa mwezi).
Kama kuna vigezo bado hujatimiza, kama kupata kitabu, wasiliana na namba 0678 977 007 kukamilisha vigezo.
KARIBU KWENYE HUDUMA.
Kama umekidhi vigezo na upo tayari kwa ajili ya kufikia UHURU WA KIFEDHA, karibu uweze kujaza fomu ya taarifa zako za msingi zitakazotumika kwenye huduma hii.
Kupata huduma hii, BONYEZA MAANDISHI HAYA na ujaze fomu kwa usahihi. Taarifa zote utakazojaza kwenye fomu zitakuwa siri kati yako na Kocha, hazitashirikishwa kwa watu wengine.
Karibu sana kwenye huduma ya STAAFU NA UHURU WA KIFEDHA uweze kujenga uhuru wa kifedha kwa uhakika kwenye maisha yako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani.
MUHIMU; Kuingia kwenye huduma, BONYEZA MAANDISHI HAYA KUJAZA FOMU.