Jumapili iliyopita ya tarehe 13/04/2014 nilikuwa mgeni kwenye kipindi cha AMKA NA BADILIKA kupitia TBC1. Katika kipindi hicho nilizungumzia mambo mengi ambayo yanaweza kumsaidia mtanzania yeyote anayetaka kubadili maisha yake kuwa bora zaidi.

amka na badilika2

  Nilizungumzia kwa kifupi historia ya maisha yangu, mafanikio makubwa niliyowahi kuyafikia na pia changamoto kubwa nilizowahi kupitia. Moja ya mafanikio makubwa niliyowahi kuyafikia baada ya kupanga kufanya hivyo ni kupata daraja la kwanza la alama tatu(DIVISION ONE POINT 3) kwenye mtihani wa kidato cha sita. Maana yake nilipata alama A kwenye masomo yote matatu ya msingi niliyosoma ambayo yalikuwa Physics, Chemistry na Biology.

  Changamoto kubwa niliyozungumzia ilikuwa ni kufukuzwa chuo kikuu mwaka 2011 na kuingia mtaani nikiwa sina mbele wala nyuma na kuona kama ndoto zangu zote zimezima. Lakini kutokana na kupambana na kutokata tamaa ndio maana leo hii naweza kukuandikia makala zinazoweza kukusaidia.

  Pia nilizungumzia biashara mbalimbali nilizofanya na ninazoendelea kufanya na chanzo cha mtaji.

  Mwisho kabisa nilizungumzia ndoto zangu kubwa za kuwa bilionea na baadae kuwa RAISI WA TANZANIA ili niweze kuwakomboa watanzania wenzangu kifikra, kimtazamo na kiuchumi.

  Ni mazungumzo ambayo unaweza kujifunza vitu vingi sana na ukavitumia kwenye maisha yako na yakawa bora zaidi. Wengi wa walioangalia mazungumzo yale wamenitafuta kwa mawasiliano na wamenipa ushauri mzuri sana.

  Kama kwa sababu moja au nyingine ulikosa kipindi hiki kilichorushwa jumapili unayo nafasi ya kukiona kipindi hiko. Kipindi kitarudiwa kesho jumatano tarehe 16/04/2014 saa nane mchana mpaka saa tisa kupitia TBC1. Pata muda ukiangalie kipindi hiki kesho.

  Kwa wale ambao hawana ukaribu kabisa na tv bado unaweza kupata maongezi ya kipindi hiki kupitia dvd. Kuna dvd za kipindi hiki na unaweza kuzipata kama unahitaji. Tumia mawasiliano yafuatayo 0755285023 kuhusu utaratibu wa kujipatia dvd.

  Nakutakia kila la kheri katika harakati zako za kuboresha maisha yako na ya wale wanaokuzunguka.

Kumbuka TUKO PAMOJA KWENYE SAFARI HII.