Unahitaji Daraja La Kukutoa Hapo Ulipo, Hivi Ndivyo Unavyoweza Kulipata.

Kwenye maisha yako unajua ni kitu gani unataka. Hata kama hutokipata na hata kama maisha yako yanakuwa magumu kiasi gani kuna kitu ambacho unakitaka na unakijua kabisa.

  Inawezekana unataka maisha bora na yenye kufurahia, inawezekana unataka kazi nzuri na yenye manufaa, inawezekana unataka utajiri pia inawezekana unataka kuwa na afya bora au kuacha kuahirisha mambo. Haya yote na mengine mengi ni mahitaji ambayo wengi wetu tunakuwa nayo.

  Kila mtu ana mahitaji yake muhimu, na mahangaiko yote tunayofanya kwenye maisha ni kwa ajili ya kufikia mahitaji haya muhimu kwetu.

DARAJA2

  Lakini pamoja na kuwa kwamba kila mtu ana mahitaji na kila mtu anajua ni nini anahitaji, bado ni watu wachache sana ambao wameweza kufanikiwa kufikia mahitaji yao. Kwa kifupi ni watu wachache sana ambao wamefanikiwa kwenye shughuli wanazofanya huku wengi wetu tukiendelea kuteseka bila ya kufikia mahitaji yetu.

  Unafikiri ni kitu gani kinawawezesha baadhi ya watu kufanikiwa kupata wanachotaka na wengine kushindwa kufanikiwa? Ni kweli kwamba wanaofanikiwa wana akili kushinda wengine? Je kuna uwezekano mkubwa kwamba wao wana bahati sana ndio maana wameweza kufanikiwa na wewe umeshindwa kwa sababu huna bahati? Kama majibu yako ni ndio, una safari ndefu ya wewe kufikia mafanikio yako, na huenda usiyafikie kabisa.(soma; kama unataka kuwa na bahati fanya hivi.)

  Kuna nafasi kubwa kati ya hapo ulipo na pale unapotaka kufika, yaani kufikia mahitaji yako kwenye maisha. Ni sawa na kuwa upande mmoja wa mto mkubwa na unataka kufika upande wa pili. Ili uweze kufika upande huo wa pili unafanya nini?

  Ili uweze kufika upande wa pili wa mto, kuna njia mbili unaweza kutumia. Moja ni kuingia mtoni na kuogelea na ya pili ni kutafuta daraja na kuvuka kuenda upande wa pili. Katika safari zetu za kufikia mafanikio kuna watu ambao wanaogelea na kuna watu ambao wanatumia daraja. Je wewe unatumia nini?

  Wanaoogelea ni wale ambao wanajua wanakotaka kufika ila hawajui ni njia ipi ya uhakika wanayoweza kuitumia kufika pale. Hivyo wanajikuta wanafanya mambo mengi na kutumia nguvu nyingi ila wanaishia kushindwa na kutofika kabisa upande wa pili. Hii ni kwa sababu kuna vizuizi vingi sana kwenye safari hiyo, kuna kukatishwa tamaa, kuna kushindwa, kuna kukata tamaa mwenyewe na kadhalika. Usisahau kuogelea pia kuna hatari kubwa ya kuliwa na mamba.

  Wanaotumia daraja ni wale ambao wanatafuta njia ya uhakika inayoweza kuwafikisha upande wa pili. Kupitia njia hii wanaweza kufika upande wa pili bila ya misukosuko mingi na hatari kubwa ya kuliwa na mamba au kuchukuliwa na mkondo wa maji na kupotea kabisa.

  Unahitaji daraja.

Ili kufikia malengo yako kwenye maisha, unahitaji daraja la kukutoa hapo ulipo na kukufikisha unakotaka kwenda. Kama mpaka sasa hujajua daraja unalotakiwa kutumia utakuwa unaogelea kitu ambacho kinaelekea kukupoteza. Daraja linaweza kuwa;

1. Wewe mwenyewe.

Kwa wewe mwenyewe kujua ni wapi ulipo na ni wapi unataka kwenda na kuangalia historia yako unaweza kujisaidia mwenyewe kufika upande wa pili badala tu ya kwenda kichwa kichwa.

2. Watu sahihi.

Ni rahisi sana kufikia mafanikio yako kama utakuwa umezungukwa na watu wenye malengo kama yako. Kama umezungukwa na watu ambao hawana malengo watakurudisha nyuma na utashindwa kufika upande wa pili.

3. Mafunzo.

Mafunzo ndio daraja bora ambalo unaweza kulitumia kufikia malengo yako. Unaweza kupata mafunzo kwa kujisomea vitabu, kutembelea mitandao kama AMKA MTANZANIA, kuhudhuria semina na hata kutafuta ushauri wa kitaalamu.

  Kwa vyovyote vile unahitaji daraja la kukufikisha upande wa pili, acha kuogelea kwa kufanya mambo ambayo hujui yatakufikisha wapi. Angalia lilipo daraja na anza kulifuata mpaka ufike upande wa pili wa safari yako ya maisha.

  KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya madaraja bora sana kwako kufikia malengo yako kwenye maisha. Jiunge na kisima cha maarifa ili upate maarifa mbalimbali ya kuboresha maisha yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu kisima cha maarifa bonyeza maandishi haya.

  Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako. Kumbuka, TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: