Leo Ndio Siku Ya Mwisho, Kama Bado Unasita Unapoteza Nafasi Kubwa Sana.

Leo ndio siku ya mwisho ya kujiunga na mafunzo ya kozi fupi ya JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Haya ni mafunzo mafupi ambayo yatakusaidia uweze kutengeneza biashara kubwa na kupata kipato kisicho na kikomo kupitia mtandao. Nasema kipato kisicho na kikomo kwa sababu juhudi zako ndio zitapima kipato chako, ukiweka juhudi kidogo unapata kipato kidogo, ukiweka juhudi kubwa unapata kipato kikubwa. Tofauti na ilivyo kwenye ajira kwamba hata uweke juhudi kubwa kiasi gani mshahara wako ni ule ule, au utaongezeka kidogo sana.

Kwa njia hii mpya unaweza kufanyia kazi popote unapotaka. Unaweza kufanyia kazi nyumbani kama kuna utulivu wa kutosha, unaweza kuwa unafanyia kazi ofisini na unaweza hata kufanyia kwenye ufukwe. Unaweza kusafiri unakotaka na bado ukaendelea kufanya kazi zako.

pesa mtandao

Kama bado unasita unapoteza nafasi kubwa.

Huenda bado unasita labda kitu hiki hakikufai, au labda huwezi kukifanya au huwezi kuandika. Uko sahihi kabisa, naomba nikuulize swali moja, ni kipi ulizaliwa ukiwa unakijua? Vitu vyote umejifunza ina maana na aina hii ya biashara pia utajifunza na kupitia kozi hii utapata misingi muhimu ambapo utaanzia kujiendeleza kidogo kidogo.

Ni vyema ukachukua hatua ya kujifunza kozi hii sasa kwa sababu unaweza usipate nafasi ya kujifunza tena hivi karibuni.

Hutopata nafasi hii kwa sababu kwa mwaka huu nilipanga kufundisha kozi fupi nne tu, ya kwanza ilikuwa JINSI YA KUWEKA MALENGO MAKUBWA UTAKAYOYAFIKIA na ilifanyika mwezi wa kwanza, ya pili ni hii na nyingine mbili zitakuja. Kwa ratiba hii ni vigumu sana kurudia kozi yoyote ndani ya mwaka huu.

Chukua hatua mapema kabla ya siku ya leo kuisha ili uweze kupata elimu hii ambayo itakuwa msaada kwako.

Kozi hii itafundishwa kwa siku kumi na itafundishwa kwa njia ya mtandao hivyo utaweza kuifuatilia popote ulipo duniani.

  Katika kozi hii utajifunza vifuatavyo;

1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.

2. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.

3. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.

4. Uandishi wa makala zenye mvuto.

5. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).

6. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.

7. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.

8. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.

9. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.

10. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.

  Kozi hii itafundishwa kwa njia ya mtandao na itachukua muda wa siku kumi tu. Gharama ya kozi hii ni shilingi elfu kumi za kitanzania.

  Kujiunga na kozi hii tuma fedha(tsh 10,000/=) na email yako kwa mpesa au tigo pesa 0755953887/0717396253 kisha utaingia kwenye kozi hii. Kozi itaanza rasmi tarehe 28/04/2014. Mwisho wa kujiunga na kozi hii leo ijumaa ya wiki hii tarehe 25/04/2014.

  Hii ni nafasi kubwa sana kwako kuweza kutengeneza kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Dunia inabadilika kwa kasi sana na mtandao wa internet umetengeneza matajiri wengi sana duniani. Usiachwe nyuma na njia hii ya kipekee na ya uhuru ya kujiingizia kipato.

  Karibu kwenye ukombozi wa maisha yako kiuchumi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: