Kwa wale ambao wamejiunga na kozi fupi ya JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG leo asubuhi nimetuma email ya kwanza kuhusiana na mafunzo haya.
Kama ulituma fedha kwa ajili ya mafunzo yako na umeangalia email yako ila hujapata email niliyotuma naomba unipe taarifa kabla ya leo kuisha.
Pia kuna watu kama watatu ambao wametuma fedha ila hawakutuma email kwa ajili ya kuwekwa kwenye kozi. Watu hao walituma fedha kwa Mpesa na mmoja kwa Airtel money. Naomba watu hawa wanitafute leo ili waweze kuingia kwenye kozi na twende pamoja.
Vinginevyo nawatakia kila la kheri wasomaji wote wa AMKA MTANZANIA wiki ijayo kuna mambo mapya yatakuwa yakitokea kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Endelea kutembelea kutembelea mitandao hii ili ujifunze na kuboresha maisha yako.
Kumbuka TUKO PAMOJA.
