Majibu Kwa Ambao Bado Hawana Uhakika na Zawadi Ya Kitabu.

Kwenye makala hii kuna vitu viwili; kwanza majibu na ufafanuzi wa maswali ambayo yameulizwa sana kuhusu kozi itakayoanza jumatatu, na pili zawadi ya kitabu kwa wasomaji wote. Hivyo twende pamoja.

Majibu na ufafanuzi kuhusiana na kozi ya kutengneza pesa kwenye mtandao kwa kutumia blog.

1. Kozi hii inaendeshwaje?

Kozi hii inaendeshwa kwa njia ya email na washiriki watatumiwa email moja kila siku kabla ya saa kumi na mbili asubuhi. Mshiriki ataisoma email hiyo muda wowote ndani ya siku husika na ikiwa ana swali atauliza kwa kujibu email hiyo na atajibiwa siku hiyo hiyo.

Email hiyo unaweza kuisoma kwenye computer au hata kwenye simu ya mkononi kama ina uwezo huo.

2. Nina Airtel Money Nalipaje?

Kama unataka kulipia kozi hii ila una Airtel money unaweza kutuma fedha moja kwa moja kutoka Airtel money kwenda mpesa au tigo pesa. Nenda kwenye kutuma pesa na uchague option hiyo.

3. Je nahitaji kuwa na blog kabla ya kujifunza kozi hii?

Sio lazima uwe na blog kwa sasa, ila baada ya kupata kozi hii unaweza kujifunza kutengeneza blog kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA au kwa anayehitaji nitamtengenezea blog kwa punguzo la asilimia 40. Kwa vyovyote vile kozi hii ni muhimu sana kwako hata kwa biashara nyingine unazofanya.

4. Je kutakuwa na mtihani na vyeti?

Linaonekana kama swali la kizushi ila kuna wanaouliza. Hii ni kozi ya kukusaidia wewe kutumia fursa zinazokuzunguka kutengeneza biashara. Kama tunavyojua karibia kila mtu anayetumia mtandao anaingia facebook ikiwemo wewe, sasa nataka ujue jinsi gani unaweza kutengeneza fedha kupitia hiyo facebook na blog yako. Hivyo sio kozi ambayo utapewa cheti bali utapewa mbinu zitakazokusaidia sana.

Wahi kujiunga na kozi hii kwa masaa haya machache yaliyobaki kabla ya siku ya leo kuisha.

pesa mtandao

Zawadi ya kitabu kizuri.

Watu wengi waliojiunga na mtandao huu siku za hivi karibuni wameniaandikia kuhusu kutopata vitaku kwanzia wamejiunga. Kwanza kabisa unapojiunga tu kuna email unarudishiwa ambayo ina link ya kitabu, nafikiri wengi wahaioni.

Kutokana na hizi natoa zawadi ya kitabu kizuri kwa wasomaji wote.

Kitabu hiki kinaitwa The Science of Getting Rich.

Kitabu hiki kinaelezea ni jinsi gani kupata utajiri na hata kufanikiwa ni sayansi. Na kama ilivyo kwa sayansi nyingine unahitaji kujua misingi ili uweze kupata unachotaka.

Misingi hiyo ndiyo imeelezewa kwenye kitabu hiki. Kama nilivyosema kwenye makala iliyopita kuhusu KUWA BILIONEA, ni muhimu sana kupata busara hizi muhimu kutoka kwa watu waliofika huko.

Pata busara hizo kwa kujisomea kitabu hiki. Hiki kitabu kina kurasa 64 hivyo unaeza kukimaliza kusoma kwenye wikiend hii.

Kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya ya kitabu The Science of Getting Rich na utakidownload moja kwa moja.

Nakutakia kila la kheri kwenye harakati zako za kufikia mafanikio.

Kumbuka TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: