Leo tarehe 02/07/2014 ni siku ya 183 kati ya siku 365 za mwaka huu 2014. Hii ina maana kwamba mpaka jana tulikuwa tumemaliza siku 182 na kuanzia kesho tumebakiza simu 182 kuumaliza mwaka huu 2014. Hii inaifanya siku ya leo kuwa ya kati kati kabisa kwa mwaka huu na itakuwa siku muhimu sana kwako kama utaendelea kusoma hapa na kuchukua hatua.

goal

Nakumbuka mwaka huu ulipoanza uliweka malengo mengi sana na ulikuwa na imani kubwa mwaka huu utakuwa mwaka wako. Ulisema utafungua biashara, utakuza biashara unayoendelea nayo, utaanza kufanya mazoezi, utapunguza starehe, utaanza kuwa na matumizi mazuri ya fedha, na mengine mengi sana ambayo ulijipangia kuyafanya mwaka huu.

Sasa naomba nikuulize swali moja, ni kipi kati ya vile ulivyopanga kufanya umefanikiwa kukifanya na hata kufikia nusu? Nina hakika ulichofanikiwa kufika nusu ni siku za mwaka huu, yaani umefanikiwa kuishi nusu ya mwaka mpaka leo. Asilimia kubwa ya malengo uliyoweka mwanzo wa mwaka huu umeshayasahau kabisa. Kuna ambayo ulianza kufanya wiki chache za mwanzoni baadae ukarudi kwenye maisha yako ya kila siku.

Ulifanya hivyo hivyo mwaka jana, mwaka juzi mwaka ule mwingine tena na imekuwa ndio tabia yako miaka kumi iliyopita.

Na kama usipochukua hatua utaendelea na tabia hii na siku moja utashtuka kama umeamka usingizini na kujiuliza swali moja ambalo litakuumiza sana na kukutoa machozi. Utajiuliza NILIISHIJE MAISHA YANGU? MUDA WOTE WA MAISHA YANGU ULIPOTELEA WAPI?

Sio kosa lako.

Kama umekuwa na tabia hii kwa miaka kumi iliyopita inaweza kuwa sio kosa lako kwa sababu kwa sehemu kubwa huwa tunaweka malengo kutokana na kwamba kila mtu anaweka malengo. Na pia mara nyingi tunaweka malengo tukiwa na hisia kali za furaha ya kuingia kwenye mwaka mpya. Mambo haya yanakufanya useme malengo bila ya kuweka mkakati wa kuyafikia.

Litakuwa kosa lako na utalijutia sana kwenye maisha yako kama umesoma hapa leo halafu usichukue hatua. Kwa kuwa utakuwa umeshajua ya kwamba umekuwa ukifanya makosa hivyo kama utaendelea kuyarudia hapo utakuwa unakosea, na siku ile utakayojiuliza maswali yatakayokusononesha utaukumbuka sana ujumbe huu.

Badili mwelekeo wa maisha yako sasa, sio mpaka tena mwaka kesho.

Najua utakuwa unasema mwaka huu nimeshindwa, ngoja nisubiri tena mwaka ujao nitaweka malengo makubwa na nitayafikia. Kabla hujaendelea na mawazo yako haya mazuri naomba nikuulize; haya si ndio maneno uliyosema mwaka jana na hata mwaka juzi? Mbona hukuyatekeleza?

Kama ulivyoshindwa kutekeleza mwaka huu, ndivyo utakavyoshindwa kutekeleza mwaka kesho na miaka mingine itakayofuata.

Leo nataka ukate mzizi wa fitina na uanze sasa, sio mwaka kesho bali siku chache zijazo ufanye mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

Mwezi wa kwanza mwaka huu niliandaa semina ya JINSI YA KUWEKA MALENGO MAKUBWA NA UTAKAYOYAFIKIA ambayo ilifanyika ubungo plaza. Baada ya pale nilifundisha tena semina hiyo kwa njia ya mtandao kwa kutumia email. Semina hizi zilikuwa na mafanikio makubwa sana kwani washiriki walijifunza vitu vizuri sana ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwenye maisha yao.

Sasa nakupatia nafasi ya kupata tena mafunzo haya kwa njia ya EMAIL. Unaweza kujifunza jinsi ya kuweka malengo makubwa utakayoyafikia kwa njia ya email. Utatumiwa masomo mazuri sana yenye maelekezo jinsi ya kufanya na utaweza kuuliza swali iwapo kuna sehemu hujaelewa vizuri. Mafunzo yataendeshwa kwa siku tano.

Kwa kupata mafunzo haya, mara moja utaanza kuboresha maisha yako badala ya kusubiri yena mpaka mwaka 2015. Siku 182 zilizobaki ni nyingi sana kuweza kubadili maisha yako.

Gharama ya mafunzo haya ilikuwa tsh elfu kumi, ila kwa sasa kwa sababu napenda watu wengi sana waweze kuyapata nitapunguza gharama yake na kufanya iwe tsh elfu tano(5,000/=). Kama unataka kupata mafunzo haya fanya kulipia mapema ili uweze kupata nafasi hii ya kuboresha maisha yako. Nafasi ya kulipia kwa bei ya punguzo itaisha ijumaa tarehe tano. Baada ya hapo gharama itaendelea kuwa tsh elfu kumi.

Mafunzo yataanza rasmi siku ya jumatatu tarehe 07/07/2014. Kulipia mafunzo haya tuma fedha tsh 5,000/= kwa mpesa au tigo pesa 0755953887/0717396253 na kisha utume email yako ili uweze kuunganishwa kwenye masomo. Ikipita ijumaa itabidi ulipe tsh 10,000/= ili kupata mafunzo haya.

Nakukaribisha sana kwenye mafunzo ambayo yatakusaidia sana kubadili mwelekeo wa maisha yako.

TUKO PAMOJA SANA.

kitabu kava tangazo