Hiki Ndicho Kitu Kikubwa Kinachozuia Kwenye Mafanikio!

MAKALA HII IMEANDIKWA NA IMANI NGWANGWALU WA TANGA TANZANIA.

Watu wengi hawana ndoto za kimaisha. Ni watu ambao wanasubiri mazingira yafungue hali na sura yoyote itakayokuja mbele yao. Hawana ndoto kwa sababu wanaamini kwamba ndoto bila kuwa na fedha ni kazi bure. Hawa wanasubiri miaka na miaka fedha ije ili wawe na ndoto lakini fedha haiji na ndoto haziji.

Nikisema ndoto nina maana ya malengo maishani. Je, ungependa kuwa nani au kufanya nini kwenye maisha yako? Kuna mahali au jambo ama hali unayoiona ambayo unaiendea na ndiyo hasa inayofanya maana ya maisha yako?

Watu wengi hawana malengo, hawaamini kwamba yanaanza malengo ndipo fedha zije. Kwao wanadhani fedha zitakuja na ndipo watakapopata malengo. Kwa hiyo ni sawa na watu kusubiri mtoto amzae baba yake.

Ukweli ni kwamba fedha si kikwazo kinachokufanya usitimize ndoto zako. Tatizo kubwa linalofanya ndoto zako zisitimie ni wewe mwenyewe.

Fedha zinatumika kama kisingizio kwa sababu ni rahisi kusema kwamba fedha ndilo tatizo lenyewe kuliko kukubali kwamba wewe ndiyo tatizo lenyewe linalosababisha ndoto zako zisitimie.

Kama unataka kuanzisha biashara, kuna rasilimali nyingi ambazo utazikuta kwenye maeneo mbalimbali, hata kwenye mitandao ambazo zitakusaidia namna ya kuanzisha biashara bila kutumia kiasi kikubwa sana cha fedha.

Fedha si tatizo la kweli lililoko mbele yako linalokwamisha mipango yako. Kitu kikubwa kinachokuzuia wewe kufikia mafanikio yako ni malengo.

Visingizio uvifanyavyo vinaficha mambo yaliyojificha ndani ambayo ni hofu na mashaka. Unatarajia kuanguka au vikwazo, kwa hiyo unakuwa na hofu ya kutimiza ndoto zako. Unaachana na ndoto hizo na kuanza kukata tamaa.

clip_image002

Huwezi kufanikiwa katika maisha kama hujiamini acha kutumia fedha kama sababu iliyokufanya kutofika pale ulipotakiwa kuwa katika maisha.

Kwa nini uishi kwa kubangaiza wakati unaweza kuishi ukiwa na mali nyingi? Unaweza kufanya mambo mengi na fedha lakini huwezi kununua ndoto zako.

Jibu ni wewe kuwa na ndoto ya maisha yako. Unataka maisha yako yaweje? Ni watu watatu au wanne tu kati ya mia moja ambao wanajiwekea malengo na kuishi kwa malengo.

Kama unataka kuzibadilisha ndoto zako na kuwa kitu cha kweli, hakuna kitu kingine. Kuongea sana hakukusaidii lolote na wala hakutakuja kukusaidia. Kuwa na malengo ndicho kitu cha msingi.

Achana na blablaa na badala yake chukua hatua zitakazokuletea utulivu utakapokuwa unatekeleza ndoto zako.

Jifunze kwenye maisha yako kuweka malengo na kuyafanikisha kwani huu ndio utaratibu mzuri na wa kuaminika.Ni utaratibu ambao utakupa furaha na mafanikio makubwa kwa muda mrefu.

Utaratibu huu utakupa uzoefu mkubwa katika mambo ya malengo, wakati mwingine utajikuta huamini unapoanza kuandika malengo mapya mara baada ya yale ya kwanza kwisha. Inakuwa inatia moyo kuanza kupanga malengo upya mara baada ya yale ya kwanza kwisha.

Nakushauri anza na malengo sema hasa ungependa kuwa nani maishani, unaona nini mbele yako baada ya miaka kadhaa.

Unaweza ukachukua umiliki wa tabia hii ya kujiwekea malengo ili ufanikiwe zaidi. Lakini hakikisha malengo unayojiwekea yawe yakufikika na si kufikirika tu.

Uwezo wa kuwa mtu mwenye mafanikio makubwa maishani mwako unao,usifanye tena kosa hili linalokuzuia kwenye mafanikio yako.Ni vyema ukachukua hatua juu ya malengo yako.

Kama kuna sehemu unakwama au unataka kuelewa zaidi juu ya malengo yako hakikisha unasoma zaidi makala. Jinsi ya kuweka malengo utakayoyafikia na Makosa makubwa matano unayoyafanya wakati unaweka malengo hapa hapa katika mandao huu wa AMKA MTANZANIA.

Mwezi huu wa saba tutaendesha mafunzo ya jinsi ya kuweka malengo makubwa ambayo utaweza kuyafikia. Mafunzo haya yataendeshwa kwa njia ya email na yatakwenda hatua kwa hatua mpaka kuweza kupata malengo mazuri. Kujiunga na mafunzo haya tuma fedha tsh elfu tano na email yako kwenye namba 0717396253/0755953887. Mafunzo yataanza jumatatu tarehe 7, mwisho wa kulipia tsh elfu tano ni kesho ijumaa baada ya hapo gharama itakuwa tsh elfu kumi. Wahi mapema kupata nafasi hii ya kubadili maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio iwe ya ushindi,

TUPO PAMOJA!

UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANDISHI WA MAKALA HII IMANI NGWANGWALU KWA 0767048035.

KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com

MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISHWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s