Habari za leo msomaji wa AMKA MTANZANIA, natumaini unaendelea vizuri na harakati zako za kuboresha maisha yako kila siku.
Naendelea kukupa moyo kwamba lolote unaloamua kufanya na kujitoa nguvu zako kulifanya lazima utafikia mafanikio makubwa.
Kwa wale ambao wamelipa fedha ili kupata mafunzo ya JINSI YA KUWEKA MALENGO MAKUBWA UTAKAYOYAFIKIA leo asubuhi wametumiwa email ya utangulizi wa masomo yatakayoanza wiki ijayo.
Kama ulilipia mafunzo haya na kutuma email yako tafadhali angalia kama umepata email ya kwanza. Kama unatumia GMAIL angalia kwenye vipengele tofauti kama PROMOTIONS au UPDATES.
Kama hujaipata tafadhali nitumie tena email yako kwa usahihi ili uweze kuingia kwenye mafunzo haya.
Kuna watu wawili ambao walituma fedha ila hawakukumbuka kituma email zao. Naomba kama na wewe ni mmoja wao nitumie email yako pamoja na meseji uliyorudishiwa baada ya kutuma fedha ili uweze kuingia kwenye mafunzo haya mapema.
Kwa wale ambao wangependa kupata mafunzo haya ila wamechelewa kulipia, unaweza kulipia leo tu kwa tsh elfu kumi. Tuma fedha hiyo, 10,000/= kwa Mpesa 0755953887 au tigo pesa 0717396253 na utume ujumbe wenye email yako na maelezo ya kwamba unataka kujiunga na mafunzo ya kuweka malengo. Baada ya leo nafasi ya kujiunga itafungwa rasmi ili kuweza kuendelea na utaratibu wa kutuma mafunzo.
Nakukaribisha sana kama ulichelewa kujiunga ujiunge sasa.
Nakutakia kila la kheri kwenye harakati zako za kuboresha maisha yako.
TUKO PAMOJA.
