Nini Maana ya World class performance?

Ufanisi wa kiwango cha kimataifa au kidunia ni pale ambapo unalifanya jambo kwa ubora wa kipekee na hii kukufanya ufikia mafanikio makubwa sana. Kwa ufanisi wa kiasi hiki ndio unakuwa bora na kuweza kuvunja au kuweka rekodi ambazo zimewahi kuwepo hapo awali.

Ni sehemu au shughuli gani unaweza kuzifanya kwa viwango vya kimataifa?

Kazi au shughuli yoyote unayoifanya unaweza kuifanya kwa viwango vya kimataifa na kufikia mafanikio makubwa sana.

Iwe unafanya kazi za usanii kama kuandika, kuimba, kuchora na hata ubunifu. Iwe unafanya biashara ya aina yoyote ile iwe jumla au rejareja. Iwe unafanya kazi za kitaalamu kama daktari, mwalimu, mhasibu, mwanasheria na kadhalika. Iwe unafanya shughuli nyingine kama kilimo, ufugaji, ushauri. Iwe unafanya michezo kama mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira wa kikapo, kukimbia mbio, kunyenyua vitu vizito, na hata kupigana. Kazi yoyote ile inayofanyika na binadamu ina uwezo wa kufanyika kwa viwango vya kimataifa.

Ukiangalia rekodi mbalimbali za dunia utaona kwenye kila nyanja ya maisha kuna watu fulani wanaoheshimika kwa ufanisi wao uliopitiliza.

Ni nani anayeweza kufikia viwango vya kimataifa?

Mtu yeyote ambaye ameamua kufanya kile anachofanya kwa viwango vya kimataifa anaweza kufanya hivyo. Hii inamanisha kwamba hata wewe una uwezo wa kufanya hiko unachofanya au unachopendelea kufanya kwa viwango vya kimataifa na kuweza kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Kwa nini world class?

Kila mtu anapenda kupata mafanikio kwenye maisha yake. Hata kama hupendi mafanikio moja kwa moja basi unapenda maisha yako kuwa bora zaidi ya hapo yalipo. Sasa kama tunataka mafanikio na tunawez kupata kile kidogo tunachotafuta kwa nini tusiende kwa vikubwa zaidi?

Kwa nini tukubali kupata vidogo wakati tunaweza kufikia vikubwa zaidi ya hapo? Hii ndio sababu kubwa iliyonifanya kuja na mpango huu wa WORLD CLASS. Katika mpango huu wa world class nahitaji kuwa na watu ambao wamejitoa kweli kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao na shughuli zao. Ndio maana hata gharama za kuingia kwenye mpango huu ziko juu kidogo ili iwe sehemu ya watu ambao wamejitoa kweli kwa ajili ya kujifunza na kushirikishana na wengine ambao wanaelekea kwenye njia moja.

Hatujaanzisha WORLD CLASS ili kuwatenga wengine ila tumeanzisha ili kujua ni wapi ambao wanayataka sana mafanikio na wako tayari kuyafikia kwa juhudi zozote. Sio wote ambao wanauhitaji mkubwa kiasi hiki wa mafanikio.

Hivyo wewe kama mmoja wa wanachama wa GOLD kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni mmoja wa watu ambao wanaelekea kwenye mafanikio makubwa sana.

Je uko tayari kwa ajili ya mafanikio makubwa?

Kama ndio chagua kitu kimoja, ndio narudia tena KITU KIMOJA TU ambacho unataka kuwa bora kabisa kwenye maisha yako na uko tayari kukifanyia kazi kila siku ili kufikia mafanikio hayo makubwa. Baada ya hapo njoo kwenye FORUMS za majadiliano na ingia kwenye forum ya WORLD CLASS PERFORMANCE na tushirikishe kile unachopanga kufanya. Kwa njia hii tunaweza kusaidiana kwenye changamoto mbalimbali tunazopitia.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii kubwa ya kufikia mafanikio makubwa.

TUKO PAMOJA.