WAHITIMU; Tenga Mwaka Mmoja na Utumie Muda Huo Kufanya Hivi.

Karibu kwenye kipengele cha ushauri kwa wahitimu ambapo kila wiki tunakuwa na makala yenye kutoa ushauri kwa wahitimu wote ambao wanataka kuboresha maisha yao.

Ni jambo ambalo liko wazi sasa ya kwamba ajira ni tatizo kubwa. Hata kama ulikuwa huamini au kujua hili wakati uko chuoni, siku chache ulizoingia mtaani utakuwa umeanza kuliona hilo wazi wazi.

usaili kazi4

Kutokana na tatizo hili la ajira kwa wastani itachukua zaidi ya mwaka mmoja ndio uweze kupata ajira, kama hata utaipata. Inaweza kuwa zaidi ya hapo kutokana na idadi kubwa ya wahitimu wapya na wa zamani ambao nao bado hawajapata ajira.

Hata kwa wale wahitimu ambao wana uhakika mkubwa wa kupata ajira kama walimu na watu wa kada za afya bado itachukua muda kidogo ndio waweze kupata ajira. Kwa kifupi  ni wahitimu wachahce sana ambao watapata kazi ndani ya mwaka huu, wengine wengi watapata kazi kuanzia mwaka kesho na wengine hawatapata kabisa.

Sasa leo nataka nikushauri kitu kimoja. Tenga mwaka huu mmoja ambao unajua uwezekano wa kupata ajira ni mdogo sana. Katika mwaka huu chagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa moyo mmoja na utakifanya kila siku ambacho kinaweza kuboresha maisha yako. Kitu hiko kiwe ni shughuli au kazi ambayo inaweza kukupatia kipato kikubwa baadae na ukasahau kabisa kuhusu kuajiriwa.

Kuna vitu vingi sana unaweza kuvifanya. Baadhi nimevieleza kwenye makala, ushauri kwa wahitimu, kama bado unazunguka na bahasha soma hapa. Na pia mengine nimeyaeleza kwenye makala; kabla hujaanza kuzunguka na bahasha soma hapa. Fungua makala hizo uzisome na utapata picha ya kitu gani unaweza kufikiria kufanya.

Sifa za kile utakachokwenda kufanya.

Ili kitu unachochagua kufanya uweze kufanikiwa na usiishie njiani inabidi kiwe na sifa zifuatazo.

1. Iwe ni kitu ambacho unakipenda kutoka moyoni. Isiwe kitu ambacho unaiga kwa sababu watu wengine wanafanya, bali kiwe kitu ambacho unakipenda sana na itakuwa bora sana kama kikiwa kipaji chako. Kama mpaka sasa hujajua kipaji chako soma makala; hivi ndivyo vipaji vilivyo ndani yako.

2. Uweze kukifanya kila siku. Ili uweze kubobea kwenye kitu au shughuli hiyo ni muhimu uweze kufanya kila siku. Namaanisha kwa siku 365 zijazo uwe unafanya au kujifunza chochote kuhusu kile ulichochagua kufanya.

3. Usisukumwe na fedha. Fedha isiwe motisha ya wewe kuchagua kufanya hiko unachotaka kufanya. Motisha iwe kuwasaidia wengi zaidi, kutumia vipaji na uwezo mkubwa ulio ndani yako, kuongeza thamani, kuboresha maisha ya wengine na kufanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi. Kama utasukumwa na vitu hivi, fedha zotakuja zenyewe.

Baada ya kuchagua kile unachotaka kufanya anza kukifanya mara moja na usiangalie nani anasema nini. Hayo ni maisha yako na wewe ndio una jukumu la kuyajenga au kuyabomoa.

Chukua hatua sasa kwa kutenga mwaka huu mmoja ambapo unaendelea kutuma maombi ya kazi kufanya kitu ambacho baadae kinaweza kukufanya usiombe tena kazi. Kwa kufanya hivi hakuna chochote unachopoteza kwa sababu bado utaendelea kutuma maombi na utakuwa na kila kitu cha nyongeza kwa sababu utajifunza mambo mapya na utaendeleza vipaji vyako.

Wakati ukiendelea kuchagua ni kipi utakifanya kwa mwaka mmoja kuanzia sasa kuna mafunzo maalumu yanatolewa kwa wahitimu wote wa sasa na wa zamani. Kupitia mafunzo haya utaweza kupata mwanga zaidi na kuwa na chaguo zuri la kitu gani unaweza kufanya na maisha yako yakawa bora zaidi.

Kama wewe ni mhitimu wa mwaka huu au miaka michache iliyopita naungependa kushiriki mafunzo hayo tafadhali bonyeza hapa na ujaze fomu kisha utapatiwa maelekezo zaidi.

Nakusihi sana utenge mwaka huu mmoja na kufanya kitu unachopenda kukifanya bila ya kuangalia nyuma na bila ya kusikiliza watakaokukatisha tamaa. Utakuja kushukuru sana baadae kwa uamuzi huu unaokwenda kuufanya leo.  Na kama utapenda kuendelea kujifunza na kujihamasisha zaidi jinsi ya kuwa bora kwa kile unachofanya tafadhali jiunge na KISIMA CHA MAARIFA na utapata maarofa mmengi ya kuboresha maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako.

TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: