Huu Ndio Ukweli Kuhusu Maisha Usiotaka Kuusikia Na Kuuamini.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA IMANI NGWANGWALU WA TANGA TANZANIA.

Ni ukweli usiofichika wengi wetu tunapoambiwa ukweli huwa hatupo tayari kuukubali. Hata inapotokea huo ukweli tunaoambiwa unakuwa unagusa maisha yetu moja kwa moja pia vile vile huwa ngumu kukubali zaidi ya kugombana na yule anayekuambia ukweli huo na kumwona mbaya.

Katika maisha kama kweli unataka kuendelea na kufanikiwa ipo haja kubwa ya wewe kubadilika na kukubali kujifunza kutokana na ukweli ambao unakuwa unalenga kubadili maisha yako na kuwa ya mafanikio.

Kumbuka kuna usemi usemao ukweli unauma, leo katika makala hii nataka nikupe ukweli ambao utakuuma lakini ukweli huu utakusaidia kubadili maisha yako na kukupa hamasa ya kusonga mbele zaidi kimafanikio. Huu ni ukweli ambao umekuwa ukiusikia lakini unausahau mara kwa mara.Ukweli huo ni upi?

Huu ndio ukweli unaouma ambao unausahau mara kwa mara katika maisha yako:-

1.Kufikiri na kutenda ni vitu viwili tofauti.

Huwezi kufanikiwa kama utakuwa unawaza tu nakusubiri ufanikiwe. Utafanikiwa kwa kuchukua hatua juu ya maisha yako na kujifunza juu ya kuweka malengo makubwa utakayoyaweza kuyafikia.

Huu ni ukweli ambao umekuwa ukiusahau mara kwa mara katika maisha yako, unawaza sana badala ya kuchukua hatua na kutenda. Kumbuka mambo mazuri hayaji kwa kusubiri bali yanakuja kwa kufanyia kazi ndoto ulizonazo. Ukisubiri sana utapoteza muda na utakuwa mtu wa kushindwa siku zote.

clip_image002

2.Maisha tunayoishi ni mafupi sana.

Huu ni ukweli ambao hutakiwi kuusahau kamwe kuwa maisha tunayoishi ni mafupi. Lakini hilo lisikutishe unatakiwa kufanya vitu vikubwa na kutimiza malengo yako ndani ya ufupi huo huo. Hutakiwi kukata tamaa au kuogopa sana kifo, fuata malengo yako. Jiwekee malengo ambayo utahakikisha utayatimiza na ili kufanikisha hili hakikisha usipoteze muda wako kwani una thamani kubwa sana kuliko unavyofikiri.

Ishi maisha yako kwa furaha huku ukiendeleza mipango yako. Ingawa inauma wakati mwingine ukijua maisha ni mafupi lakini usijali kifo sio hasara kubwa maishani, hasara kubwa kuliko zote katika maisha yako ni kukata tamaa. Unapokuwa unakata tamaa inakuwa kama umekufa huku ukiendelea kuishi. Mipango na malengo yako yote unakuwa umeizika, unakuwa upo upo tu hueleweki hiyo ndio hasara kubwa.(Soma pia Hivi ndivyo unavyokufa na miaka 35 na kuzikwa na miaka 65)

3.Unaishi maisha unayojitengenezea mwenyewe.

Hakuna mtu ambaye mwenye uwezo wa kuamua hatima ya maisha yako zaidi yako wewe mwenyewe. Jifunze kuwa dereva wa maisha yako. Wewe ndiye mwamuzi wa mwisho unataka maisha yako yaweje. Asije akakudanganya mtu kwamba anataka kuboresha maisha yako huo ni uongo tena uongo mkubwa. Uchungu wa maisha yako unatakiwa kuujua wewe mwenyewe.

Kama hutaki kufanikiwa acha maisha yako yawe mikononi mwa watu wengine kwa hili nakupa uhakika utakufa maskini. Wapo watu ambao akili yao yote wanategemea serikali au shirika wanalofanyia kazi liwatoe kwenye umaskini, kama una mawazo kama haya kuwa makini sana. Hakikisha unafanya maaamuzi sahihi juu ya maisha yako wewe mwenyewe. Uchaguzi upo mikononi mwako uwe tajiri au maskini.

4.Kila kitu kinabadilika kila wakati.

Maisha unayoishi hayakusubiri,maisha yanabadilika kila siku na kwa kasi ya ajabu. Kama utakuwa ni mtu wa kusubiri subiri na kuacha malengo yanapita utaachwa mbali sana katika maisha. Usisubiri kitu fanya jambo kubwa katika maisha yako.

Kama wewe unalala, huumizi kichwa juu ya maisha yako, elewa kabisa wapo watu upande wa pili wa Dunia ambao hawalali kila wakati wanawaza kipi wafanye ili waboreshe maisha yao na kusonga mbele. Unachotakiwa kufanya ili uweze kuaendana na mabadiliko haya ni wewe mwenyewe kwanza kubadilika.

Chukua hatua muhimu ya kubadilika na kujifunza juu ya kukabiliana na changamoto za mwendo kasi wa Dunia. Jifunze juu ya ujasiriamali na kujua mbinu mbalimbali za biashara ikiwemo na namna ya kutafuta masoko. Acha kutumia mbinu zile zile kila siku katika biashara yako utakwama. Kama hujui hili sana unaweza kuwasiliana nasi utapata msaada wa moja kwa moja.

5.Makosa ni sehemu ya mafanikio.

Huu pia ni ukweli ambao unausahau sana katika maisha yako. Makosa katika safari ya mafanikio hayaepukiki. Kama wewe unaogopa kukosea hautafanikiwa sana. Ili kushinda kutokuogopa makosa unatakiwa ujifunze kuwa rafiki wa makosa kwa kujifunza kila unapokosea. Yafanye makosa yawe shule au fundisho kwako utaona faida yake.

Hakuna mafanikio yoyote yanayokuja bila kukosea. Watu wote wenye mafanikio makubwa Duniani ni wale waliofanya makosa makubwa na kujifunza. Anza kuyachukulia sasa makosa yako kama sehemu ya mafanikio usiumie unapokosea hiyo ni sehemu muhimu sana ya kukua kimafanikio endapo utaijua.

6.Unaishi na watu wasiopenda kuona unafanikiwa sana.

Huu ni moja ya ukweli unaopaswa kuujua hata kama utakuuma. Unaishi au unazungukwa na watu ambao wana vijicho, husuda na fitina ambao hawapendi sana mafanikio yako ingawa sio wote.

Watu hawa wanaweza wakawa ndugu zako au rafiki zako ambao umeishi nao kwa miaka mingi ila hawapendi kuona mafanikio yako. Kitu kikubwa walichofanya ni kukuzuia usijue hilo.

Hawa ni watu ambao hupaswi kuwachukia katika maisha wapo ingawa inaweza isiwe rahisi sana kuwajua moja kwa moja. Unachotakiwa kufanya ili usiweze kuumizwa ni kuwa makini na watu hawa. Na ili uweze kuwa makini nao ni lazima uwajue watu hawa na waepuke katika maisha yako. Chukua tahadhari na kukabiliana nao ila hakikisha wasikukwamishe.

Huu ndio ukweli unaouma lakini unausahau sana katika maisha yako.Chukua hatua juu ya maisha yako na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA. Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya kuboresha maisha iwe ya ushindi kwako.

TUPO PAMOJA.

UNAWEZA KUWASILIANA NA MWANDISHI WA MAKALA HII IMANI NGWANGWALU KWA 0767048035.

KAMA NA WEWE UNA MAKALA NZURI ULIYOANDIKA NA UNAFIKIRI INAWEZA KUWAAMSHA WATANZANIA TAFADHALI NITUMIE KWENYE amakirita@gmail.com

MAKALA ISIWE IMEWEKWA KWENYE BLOG AU CHOMBO KINGINE CHA HABARI, IWE IMETUMIA KISWAHILI RAHISI NA KINACHOELEWEKA NA IWE NA MANENO KATI YA 500 NA 1000 KARIBU SANA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s