Vitabu hivi vitatu, RICH DAD, POOR DAD, THINK AND GROW RICH na THE RICHEST MAN IN BABYLON ni vitabu vizuri sana kuweza kufungua mawazo yako na kubadili mtazamo wako kuhusu maisha na hata mafanikio.

Ni vitabu ambavyo nimekuwa navituma kwa watu kwanzia mwishoni mwa mwaka 2012. Mpaka sasa nimeshatuma vitabu hivi kwa watu zaidi ya elfu moja walionitumia email zao kupitia mitandao mbalimbali.

RICH2THINK2

Pamoja na kutuma vitabu hivi kwa watu wengi sio wote ambao wameweza kuvisoma, ni wachache sana ambao watakuwa wamefanya hivyo.

Pamoja na kushindwa kuvisoma kutokana na sababu mbalimbali bado kuna wengine ambao wameshindwa kuvisoma kutokana na lugha. Wengi wamekuwa wakiniandikia kuhusiana na lugha inavyowakwamisha kusoma vitabu hivi na kupata mambo hayo mazuri.

Kutokana na changamoto hizi nimeanzisha utaratibu wa kujadili vitabu vyote muhimu ambavyo nilishawatumia na naendelea kuwatumia watu kwenye AMKA MTANZANIA. Uchambuzi huu utakuwa kwa lugha rahisi ya kiswahili hivyo kila anayetaka atapata nafasi nzuri sana ya kujifunza.

Kwa kuanza tutachambua vitabu hivyo vitatu na vikiisha tutakwenda kwenye vitabu vingine.

Lengo kubwa ni kujifunza na kuweza kuyatumia yale tunayojifunza kwenye maisha yetu ili yaweze kuwa bora zaidi na tuwezae kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Uchambuzi huu wa vitabu utakuwa unafanyika kwenye KISIMA CHA MAARIFA, na utafanyika mara mbili kwa wiki, alhamisi na ijumaa. Uchambuzi huu utaanza wiki ijayo tarehe 14/08/2014 tutaanza na kitabu kimoja na kinapoisha tunakwenda kingine.

Hii ni nafasi nzuri sana kwako kujifunza na kuboresha maisha yako.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA sasa kwa uanachama wa SILVER ili uweze kupata mambo haya mazuri. Kujiunga bonyeza maandishi haya ya KISIMA CHA MAARIFA soma maelekezo, jaza fomu kisha tuma ada ya uanachama kwenye namba0717396253/0755953887. Ada ya uanachama wa SILVER ni tsh elfu thelathini kwa mwaka ila kwa wiki hii kuna punguzo la bei ambapo itakuwa tsh elfu 20.

Usikose nafasi hii ya kipekee ya kujifunza na kuboresha maisha yako.

Karibu sana kwenye mafunzo haya ya uchambuzi wa vitabu.

TUKO PAMOJA.